Gorofa la mkombozi fishing and marine tansport lateketea kwa moto mkoan Mwanza.soma zaid
Sehemu ya ghorofa ya tano ya jengo la Kampuni
ya Mkombozi Fishing and Marine Transoprt
lililopo Kirumba Mwaloni katika Manispaa ya
Ilemela mkoani Mwanza imeungua kwa moto
ambao chanzo chake bado hakijafahamika.
Jengo hilo linalomilikiwa na mfanyabiashara wa
jijini Mwanza Kitana chacha ujenzi wake bado
haujakamilika.
ITV ilifika katika eneo la tukio hilo na kukuta
wananchi wakishirikiana na askari wa jeshi la
zimamoto na uokoaji Mwanza kuzima moto huo
uliokuwa umeteketeza mbao zinazotumika kwa
ujenzi wa ghorofa hilo, huku Afisa mafunzo na
habari wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa
Mwanza Mkaguzi Msaidizi Gadaffi Masoud
akifafanua kuhusu tukio hilo.
Tukio hilo la moto limekuja ikiwa ni wiki tatu
baada ya moto mkubwa kuteketeza sehemu ya
nyuma ya nyumba ya kulala wageni ya
Shinyanga iliyopo mtaa wa Lumumba jijini
Mwanza na kusababisha kifo cha mmiliki wa
jengo hilo Maduhu Masunga maarufu kama mzee
Shinyanga pamoja na kuteketeza silaha
mbili,kiasi kikubwa cha fedha na mali mbalimbali
ambazo thamani yake.picha kwa lisani ya itv.
0 comments :
Post a Comment