Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, July 30, 2017

Tetemeko dogo la ardhi limetokea karegwe Kagera.soma zaid


Tetemeko lililodumu kwa takriban sekunde tano
limetokea leo, Julai 30 saa nne asubuhi katika
Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kayanga wilayani
Karagwe, lakini hakuna madhara yaliyoripotiwa
kutokea.
Ofisa wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Gabriel
Mbogani amesema ili kupata uhakika wa
tetemeko hilo ni lazima kukusanya taarifa kwenye
mitambo.
Amesema wananchi mkoani Kagera kwa sasa
wapo makini baada ya kupatiwa semina kutokana
na tetemeko la Septemba mwaka jana ambalo
lilisababisha madhara makubwa.
“Wananchi wa Bukoba baada ya semina tulizotoa
na kuwaonyesha ramani ya matukio ya tetemeko
wamekuwa na uelewa, hivyo hata likitokea dogo
kiasi gani lazima watoe taarifa,” alisema
Mbogani.
Hata hivyo, amewataka wananchi kuendelea
kuchukua tahadhari kwa kuwa haijulikani ni muda
gani tetemeko kubwa linaweza kutokea kwa
kuwa uzoefu ni kuwa huanza dogo na baadaye
kuwa kubwa.
Mkazi wa mji mdogo wa Kayanga, Elieth Kikaka
amesema alitoka nje ya nyumba baada ya
tetemeko hilo kwa kuwa yamekuwa yakitokea
mara kwa mara mkoani Kagera hivyo linapotokea
ni lazima kuchukua tahadhari.
Mwisho

0 comments :

Post a Comment

Back To Top