Thaban Kamsoko amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na klabu ya Yanga.soma zaid
Klabu ya Yanga imemsainisha mkataba mpya wa
miaka miwili kiungo Mzimbabwe, Thaban
Kamusoko huku pia ikimsajili kipa wa Serengeti
Boys, Ramadhani Kabwili.
Taarifa iliyotolewa na Yanga kupitia Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika ni kwamba
Kamusoko ameongeza mkataba huo baada ya
kufikia makubaliano ya mambo kadhaa.
Katika kuimarisha lango lao, Yanga pia imefanya
usajili wa Kabwili ambaye alikuwa na Serengeti
Boys katika michuano ya Vijana Afrika mwaka
huu nchini Gabon.
Usajili umeifanya Yanga kukamilisha usajili wa
nyota wanne wapya ambapo awali ilimsainisha
kipa wa African Lyon, Youthe Rostand, beki
Abdallah Shaibu pamoja na mshambuliaji Ibrahim
Ajib.
0 comments :
Post a Comment