Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, August 16, 2017

Mzee Majuto ametangaza rasimi kustaafu kuigiza ili kurudi kumcha Allah.soma zaid

Mchekeshaji na Muigizaji maarufu wa filamu
nchini Tanzania, Alhaji Amri Athumani almaarufu
Mzee Majuto ametangaza rasmi kustaafu kazi
hiyo baada ya kuitumikia kwa zaidi ya ,miaka 30.
Mzee Majuto
Mzee Majuto amesema amechukua maamuzi
hayo baada ya kuona umri unaenda na uwingi wa
changamoto wa kazi hiyo hivyo ameamua arudi
kwenye kilimo na kumtumikia Mungu.
“Kwa sasa hivi mimi sanaa basi , nasema kwa
kweli sanaa basi labda kutokee mtu anahitaji
nimfanyie tangazo lake nikimaliza narudi
shambani kwangu nimtumikie mwenyezi Mungu
nimuombe toba kwa sababu tuliofanya ni mengi
na kuna mazuri na mabaya na mabaya ndiyo
yanayotawala kwenye maisha ya ujana kwa hiyo
tumuombe toka Mwenyezi Mungu, kwani wakati
ndiyo huu ukisema upange siku kila siku
utapanga” ,amesema Mzee Majuto kwenye
mahojiano yake na gazeti la Habari Leo.
Licha ya kustaafu Mzee Majuto ameishauri
serikali ijenge kambi nyingi za JKT ili kupunguza
idadi ya vijana wanaokaa bila kazi mitaani.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top