Home
Unlabelled
kanuni mpya za maudhui ya mitandao.soma zaid
kanuni mpya za maudhui ya mitandao.soma zaid
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Ole Gabriel anakaribisha wageni katika kikao hiki muhimu na kuwashukuru wadau kujitokeza. Hatukutaka kujifungia ndani na kuja na kanuni zetu, bali tumeamua kuita wadau tujadiliane.
Habari ina nguvu, pasipokuwa na kanuni nzuri, mifumo na msingi madhubuti inaweza kuwa hatari. "Ni lazima tuwe na kanuni ambazo zitaangalia maudhui ya ndani na kuepuka mambo ya kigeni".
Nataka kanuni hizi zihakikishe vyombo vya habari vinawapa haki ya kupata habari wenye mahitaji maalumu. Uhuru wa mitandao lazima uwe na mipaka yake ili usibugudhi au kuwadhuru watu wengine.
Kanuni za Maudhui Mtandaoni zitawahusu wenye; Blogs, Apps, Forums, Internet Cafe, waendeshaji Social Media Accounts na watumiaji wa mitandao
Kanuni zinataka wamiliki; Kujisajili, Kutoa maelezo ya wanachokifanya, Kuondoa taarifa zinazoenda kinyume na sheria ndani ya saa 24
''Msidanganyike kulilia uhuru usio na mipaka, najua kuna mataifa yanachochea uhuru huo, msifuate maneno yao"
Mitandao imekuwa ikitoa habari kwa harakati lakini inatumiwa vibaya, kuanika siri za watu na kushambulia serikali. Tunaweka kanuni hizi ili mtumie mitandao hiyo kwa mujibu wa maslai ya kuhabarisaha huku mkiwa salama.
Kuanzia saa kumi na moja asubhui hadi saa tatu usiku, hakuna kurusha maudhui ya nje, iwe muziki au habari.
Radio na TV nyingi huweka muziki kuliko vipindi vya kuelimisha, sasa ni lazima 2% ya vipindi viwe vya kuelimisha
Katika Kanuni mpya, Kituo cha habari kitatakiwa kuwa na vipindi vingi vya Tanzania kuliko vya nje. kwa Muziki, wapige 80% ya wanamziki wa Tanzania
Atakayekiuka Kanuni maudhui mitandaoni, faini yake si chini ya Sh 5 milioni au kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote" - Dk Filikunjombe
Bloga lazima asajiliwe na achuje baadhi ya taarifa, pia awe tayari kuwataja wanaompa taarifa wakati wowote atakapotakiwa.
Kwa wamiliki wa internet cafe, lazima aandike kuwa video na picha za ngono haziruhusiwi, pia atatakiwa kuweka kamera(CCTV) kwenye cafe yake.
Kwa watumiaji, uhakikishe una uhakika na unachokiandika mtandaoni, vilevile simu au kompyuta yako haviwezi kutumiwa na mtu mwingine.
0 comments :
Post a Comment