polisi wamshilia mwanafunzi wa chuo cha IFM kwa kumiliki Bastola.soma zaid
Polisi Dar wanamshikilia mwanafunzi wa chuo cha IFM mwaka wa tatu mkazi wa Segerea anayeitwa Robson Isack Maji kwa kukutwa na bastola aina ya Beretta ikiwa na risasi 6 ndani ya magazine Polisi walipata taarifa kuna watu hukodisha silaha kwa majambazi ili wafanye uhalifu na kisha walipwe fedha, ndipo walipoanza kufuatilia na kumnasa mwanafunzi huyo , katika maelezo ya awali anadai silaha hiyo na pia angeiuza kwa shilingi milioni mbili na nusu na alikuwa ameiiba kwa baba yake anayefahamika kwa Isack Maji ambaye pia sio mmiliki halali wa silaha hiyo, amabye polisi imemkamata pia. Mshitakiwa amekiri kosa hilo na amemtaja Patrick Makai ambaye pia polisi wamemkamata kama mshirika wake kwenye kukodisha silaha kwa majambazi. Polisi mpaka sasa wanamtafuta mmiliki halali wa silaha hiyo. Polisi pia wamekamata gari ya wizi lenye usajili wa T364 DJV Noah Nyeupe huko Mbezi, Polisi wanawashikilia Mustapha Hassan Mkazi wa Kimara Mwisho Athuman Peter Ngosha mkazi wa Kivule na wamebaini watuhumiwa waliiba gari hiyo tarehe 21/09/2017 kwa mtu anayefahamika kwa jina la Shoo huko Bunju na bado wanamtafuta mtuhumiwa mmoja aliyefanikiwa kukimbia Pia polisi imewakamata watuhumiwa 203 kwa kupatikana na pombe haramu ya gongo na madawa ya kulevya aina ya bangi, lita 1,479 za gongo na mitambo 14 ya kutengeneza pombe hiyo pia vimekamatwa Pia polisi wamekamata vyombo vya usafiri kwa makosa 11,374 na kukusanya faini kiasi cha Shilingi 33,9510,000 kutokana na makosa hayo -
0 comments :
Post a Comment