Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Tuesday, February 28, 2017
Kimenukaa: Wabunge wamlipua Steve Nyerere baadhi wakataa kuombwa msamaha.soma zaid

Kimenukaa: Wabunge wamlipua Steve Nyerere baadhi wakataa kuombwa msamaha.soma zaid

Kusambaa kwa sauti iliyorekodiwa mazungumzo ya mwigizaji Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ na mama wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu halijafutika, mengine yamefumka kwani baadhi ya wabunge waliotajwa kwenye sauti hiyo wamelimpua Steve. Mbali na wabunge kutajwa katika sauti hiyo iliyosambaa wiki iliyokatika, wasanii pia walitajwa ambao ni Khaleed Mohamed ‘TID’, Romeo George ‘Rommy Jones’ na Ahmed Hashim ‘Petit Man’. Kwa upande wa wabunge ni Goodluck Millinga (CCM-Ulanga), Ahmed Shabiby (CCM-Gairo), Joseph Musukuma (CCMGeita Vijijini), Freeman Mbowe (Chadema-Hai) na Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo, Kigoma Mjini). Steve pia aliwataja mawaziri wawili. Steve alisikika akiwataja wabunge hao akimwambia mama Wema kuwa, aliwafuata bungeni mjini Dodoma, Februari 6, mwaka huu ili wamsaidie bintiye aliposhakiliwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar ‘Sentro’ kwa madai ya kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, ikiwemo kukutwa na bangi. STEVE AOMBA RADHI WOTE Hata hivyo, baada ya sauti hiyo kusambaa mitandaoni Februari 23, mwaka huu na kuwa gumzo, Jumamosi iliyopita, Steve alifanya mkutano na waandishi wa habari katika Jengo la Millennium Tower, Kijitonyama na kuwaomba radhi wote aliowataja huku akikiri sauti ni yake na kwamba, hakuzungumza nao kama ‘alivyomwongopea’ mama Wema bali aliwataja katika hali ya kudumisha ukaribu wake na familia ya mama huyo. UWAZI NA WABUNGE Baada ya mkutano huo, Uwazi liliwatafuta wabunge hao, kasoro Mbowe hakupokea simu, na waliopatikana walikuwa na haya ya kusema: SHABIBY: “Steve Nyerere namfahamu. Lakini sina ukaribu naye. Niliwahi kukutana naye muda mrefu kwenye hoteli yangu ya Moleno, Dodoma. “Nakumbuka alikuja na mwanamuziki Ray C (Rehema Chalamila), lakini baada ya hapo sijawahi kuonana naye popote maana hata baada ya kukutana naye sikuwahi kuwasiliana naye. “Kuhusu kunihusisha mimi katika sakata la Wema, yale mazungumzo nimeyasikia vizuri. Si kweli alichokisema eti alikuja kukutana na Musukuma kwenye hoteli yangu na mimi nikiwepo. Ni uongo mtupu. “Sijaonana na Steve Nyerere katika siku za hivi karibuni na sijazungumza naye lolote lile hata kwa njia ya simu,” alisema Shabiby. MILLI NGA: “Ninafahamu kila kitu kinachoendelea, maana Steve Nyerere ni mtu ambaye tunakutana mara kwa mara, ukizingatia ni kada mwenzangu kwenye Chama Cha Mapinduzi. Kuhusu yeye kunishawishi mimi kumtetea Wema bungeni, jambo kama hilo halipo maana sikuwahi kukutana naye kabla ya mimi kuzungumza bungeni. “Ila baada ya bunge, jioni nilikutana naye, akaniambia kuwa, nilichokiongea ni kama nilitazama kilichokuwa moyoni mwake. Hata hivyo, nimemsamehe maana ameomba radhi kwenye mkutano na waandishi wa habari!” ZITTO: “Mimi siwezi kusemea jambo hilo maana mimi kwangu halina maana yoyote.” MUSUKUMA: “Nisikilize vizuri mwandishi, mimi Steve Nyerere hana mchango wowote kwenye maisha yangu. Mimi ni Mbunge wa Geita Vijijini na sifanyi kazi yangu ya ubunge kwa kushawishiwa na mtu. “Steve Nyerere anaweza kunishawishi mimi kwa kipi? Ngoja nikwambie kitu, kinachoendelea ni kiki ya Steve Nyerere na watu wake maana kama umesikia ile ‘place’ na waandishi aliyoitisha, anasema Makonda ni rafiki yake, sasa unaweza kupima kinachoendelea hapo.” MUSUKUMA AKATAA RADHI YA STEVE Alipoulizwa kuhusu radhi aliyoiomba Steve Nyerere kwa wote aliowataja yeye ameipokeaje, alisema: “Kama ameomba radhi basi amewaomba wananchi wangu wa Geita waliyoniweka kwenye nafasi yangu kwa lengo la kuwatetea wananchi na si kufanya kazi kwa ushawishi wa mtu.” TID KWENDA KORTINI? Taarifa zaidi zilisema kuwa, Mbongo Fleva, TID anajipanga kumfikisha Steve kortini baada ya sauti yake kumtaja akisema anamchukia sana yeye huku pia kukiwa na habari kwamba, baadhi ya wanasheria jijini hapa wamepanga kujitokeza kwa waliotajwa ili kuangalia uwezekano wa kumfungulia kesi mama Wema ambaye anatajwa na Steve mwenyewe kuwa, ndiye aliyemrekodi.

Makubwa haya...Mkuu wa wilaya akataza watu kula kitimoto kisa hiki hapa.soma zaid

Makubwa haya...Mkuu wa wilaya akataza watu kula kitimoto kisa hiki hapa.soma zaid

Walaji wa nyama ya nguruwe ‘kitimoto’ wilayani Kalambo mkoani Rukwa watakikosa kitoweo hicho kwa muda usiojulikana baada ya Serikali kupiga marufuku watu kula nyama hiyo. Hatua hiyo imefikiwa baada ya nguruwe 150 kufa kwa ugonjwa wa mafua wa African Swine Fever na kuwaacha wengine wakiwa hoi. Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Julieth Binyura alisema ugonjwa huo ulijitokeza miezi mitatu iliyopita kwenye Kitongoji cha Masazi na kusambaa katika kata za Legezamwendo na Mambwe Nkoswe. Ofisa Mifugo wa Wilaya ya Kalambo, Wilbroad Kansapa alisema nguruwe wote wanaozagaa mitaani watakamatwa na mizoga yote ifukiwe.

Wema sepetu: Hiki ndio kitu ninachokipenda zaid katika harakati zangu.soma zais

Wema sepetu: Hiki ndio kitu ninachokipenda zaid katika harakati zangu.soma zais

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye wiki iliyopita amekihama chama chake cha muda CCM na kuingia CHADEMA amefunguka na kusema kuwa anaipenda sana siasa na siku akifanikiwa katika siasa atafurahi sana kwa kuwa ni kitu anachokipenda sana. Wema Sepetu kupitia account yake ya Twitter amesema ameamua kuhama CCM na kuingia CHADEMA ili kupigania uhuru pamoja na demokrasia ambayo anahisi kwamba imeanza kupotea nchini Tanzania. "Hicho ndicho tunachokwenda kupigania, uhuru tuliokuwa nao pamoja na democracy tunayoanza kuipoteza. God guide us. Hujajua tu ni jinsi gani siku nitakapofanikiwa kuwa mwanasiasa nitakavyo furahi... Naipenda siasa sana Maybe ni roots za Daddy" aliandika Wema Sepetu Mbali na hilo Wema Sepetu anasema sasa hivi amekuwa na amani na furaha moyoni mwake. " Saizi nina amani ya ajabu moyoni mwangu... I thank my Good Lord... Kweli kila kitu katika maisha hutokea kwa sababu, saizi niite kamanda " alisisitiza Wema Sepetu

Mkuu wa shule ya sekondari ajinyonga Singida sababu ni nini?.soma zaid

Mkuu wa shule ya sekondari ajinyonga Singida sababu ni nini?.soma zaid

Mkuu wa Shule ya Sekondari Tumuli katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida, Richard Makala (58) amejinyonga kwa kamba kutokana na kile kinachodhaniwa ni upweke. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, amesema mjini Singida kuwa Mkamala alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa vipande vya chandarua iliyofungwa juu ya mti umbali wa mita 130 kutoka nyumbani kwake. Aidha kamanda huyo alisema chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba hakuna mtu au watu wanaoshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuongeza kuwa polisi inaendelea na upelelezi kubaini kilichomsibu mwalimu huyo. Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mabruki Ng’ui ameliambia gazeti la Habarileo Jumatatu hii kuwa mwalimu huyo alikuwa anaishi peke yake kwa muda mrefu baada ya mkewe ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Tanzania (KKKT) Kitusha wilayani Iramba kuamua kutengana naye kutokana na unywaji pombe. “Huyu bwana amekuwa kwenye ndoa ya jina tu maana mke wake amekuwa akiishi mbali naye kwa kipindi kirefu sana, amekuwa mpweke kwa muda mrefu mno huenda hicho ndicho kilichosababisha ajitoe roho yake,” amesema Mjumbe huyo wa Bodi. Marehemu Makala ni mzaliwa wa kijiji cha Ndago, wilayani Iramba na anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake, ameacha mjane na watoto watano.

Mpende anayekupenda asiyekupenda kwanini uumie kwa ajili yake? fahamu kilichomkuta huyu.soma zaid

Mpende anayekupenda asiyekupenda kwanini uumie kwa ajili yake? fahamu kilichomkuta huyu.soma zaid

Ili mapenzi yaweze kuwa bora kwa kila aliye katika mahusiano, huwa ni vyema kila mmoja kuiona thamani ya mwenzake. Ukipenda kujiangalia mwenyewe si ajabu mwenzako kupata hisia za kuwa humthamini wala humjali. Muunganiko wenu katika mapenzi maana yake tayari mmekuwa kitu kimoja. Katika mimi unaweka sisi. Ila pia ni vyema ikakumbukwa ladha na maana halisi ya mapenzi ipo kwa anayekupenda na kukuthamini. Unapokuwa na uhakika kama anakupenda na kukuthamini hapo ndipo nafsi yako itatulia na kuwa na amani. Ndani ya mapenzi na mtu wa aina hii ni amani na utulivu kwa kwenda mbele. Hakuna majuto wala majonzi ya kila siku. Unapoamua kuwa katika mahusiano na mtu ambaye hakupendi, bali unakuwa naye kwa kuwa tu unampenda jua umejiingiza katika utumwa. Mapenzi ni suala la kihisia zaidi. Mwenzako anapokosa hisia na wewe maana yake hata uwepo wako hauthamini inavyopaswa. Na hapo ndiyo tunaona yale mahusiano ya kingono yanapozaliwa na si ya kimapenzi kwa maana halisi. Yaani mwenzako anapokuwa na mihemko ya kingono ndipo anapokutafuta na si vinginevyo. Niliwahi kuongea na msichana mmoja aliyewahi kuniambia anampenda kijana mmoja ambaye anauhakika kabisa yeye hampendi. Alinambia uhakika huo kaupata kutokana na kijana huyo kumtakia kuna msichana yupo anampenda na kumjali ila si yeye. Kuonesha zaidi kumpenda msichana yule mwingine, jamaa aliwahi kumwambia kama ikitokea hata huyu msichana akagombana na yule mpenzi mwingine wa yule jamaa, kijana yule alikuwa radhi kumdhuru huyu msichana. Hata kwa matazamo wa haraka hapo unaweza kugundua ni kwa namna gani huyu msichana alikuwa haitajiki. Ila cha kushangaza msichana huyu(aliyeongea na mimi) alimwambia mvulana husika yuko radhi kuwa naye hivyo hivyo. Aliamua kuwa hivyo akiamini ipo siku jamaa atamuelewa. Kweli walikuwa pamoja. Ila unajua kinachomkuta sasa? Kila jamaa anapogombana na yule msichana mwingine anamtumia huyu kingono na mambo mengine yasiyo ya kimapenzi, na bila kutafakari mara mbili huyu msichana anafanya kwa kile anachoamini hali hiyo itamfanya huyu jamaa amfikirie zaidi. Kuna kitu cha kuangalia hapa. Suala la mapenzi si suala la kuoneana huruma wala aibu. Mapenzi ni hisia. Unapojitoa kwa mwenzako kwa kila jambo na unamuona haelekei ujue hana hisia na wewe. Kwanini unakubali kuteseka na kuumia kila siku kwa kumuangalia yeye tu? Ndiyo, unampenda sana, unamjali sana na unamuhitaji sana, ila kama yeye hakutaki wa kazi gani? Ni muda wa kujiangalia na wewe sasa. Ona thamani yako kama binaadamu, jionee huruma jinsi unavyoteseka kila siku kwa mtu asiyeona thamani yako. Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani, bila kujali muonekano wala rangi yako. Unahitaji mwenye kukuthamini na kukujali na si anayekufanya kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa utumwa wa mapenzi kwa kuiona thamani yako. Ni vyema ukalia kwa kumkosa kuliko kuonekana unaye wakati moyoni siyo wako. Hakuna sifa ya kuwa na mtu mwenye fedha au muonekano mzuri ikiwa hakujali wala haupo moyoni mwake. Mapenzi ni amani na raha. Mapenzi hufanya watu wafurahi na kusahau shida zao. Ila jiulize kwanini kwako hayako hivi? Unaenda kwa mwenzako badala afurahie uwepo wako, yeye anaona unajipendekeza. Unampigia simu na kumpa maneno mazuri ya faraja, yeye anaona unamsumbua. Sasa wa kazi gani? Siku njema wapendwa.
Sunday, February 26, 2017
no image

Mbunge wa Babati mjini CHADEMA anusurika kifi sasa yuko ICU

Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya ambapo mmbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira luhaga mpina wilayani babati mkoa wa manyara. Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mmbunge huyo na kulazimika kumsubiri naibu waziri ambaye ameingia kumuona mbunge Gekul na hapa naibu waziri Mpina anaeleza. Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira akalamika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwaajili ya kubebbea taka lenye dhamani ya zaidi ya milioni 200

Wachawi  wapanga kumuondoa Rais wa marekani Donard Trump madarakani.soma zaid

Wachawi wapanga kumuondoa Rais wa marekani Donard Trump madarakani.soma zaid

Wapinzani wengi wa rais wa Marekani Donald Trump, wanaamini kuwa itawabidi wasubiri kwa miaka minne ili aweze kuondoka madarakani. Lakini wachawi nchini Marekani hawakubaliani na hilo. Usiku wa manane siku ya Ijumaa, wale wanaoamini uchawi kote nchini Marekani, waliandaa matambiko yenye nia ya kumuondoa Trump uongozini. Hadi sasa ukurasa wa Facebook wa matambiko huyo umepata wafuasi 10,500. Hatua hizo zimezua ghadhabu kotoka kwa wakirsto ambao wamewalaumu wachawi hao wa kutangaza vita vya kiroho. Wachawi hao wanapanga kurudia tambuko hilo hadi pale Trump atakapoondoka ofisini. Tambiko lingine litafanyika machi 26. Chama cha wakiristo nacho kilitangaza tarehe 24 mwezi Februari kama siku ya maombi ya kuukabili uchawi huo. Hata hivyo Trump hajazungumzia lolote kuhusu vita hivyo kati ya kanisa na uchawi.

Back To Top