MICHEZO
BURUDANI
SIASA & JAMII KWA UJUMLA
Recent Post
Hii ndilo jina jipya la pombe za viroba ambapo jina hilo jipya ni Nguruka ni wapi hapo.soma zaid
WAFANYABIASHARA wa vileo mkoani Morogoro, wamebadili jina la pombe inayofungashwa katika mifuko ya plastiki maarufu viroba kwa kuiita ‘nguruka’ kukwepa mkono wa sheria. Nguruka ni jina ambalo linatumika kwa wenyeji kuogopa kutaja jina la kiroba na linajulikana kwa wengi katika Manispaa ya Morogoro na vitongoji vyake. Katika baadhi ya mitaa, MTANZANIA limebaini kwa sasa watumiaji wa pombe hizo wamebuni jina hilo waweze kuendelea na biashara hiyo bila kujulikana na vyombo vya dola na mamlaka nyingine zinazohusika na ukamataji huo. Mmoja wa watumiaji wa kinywaji hicho aliyejitambulisha kwa jina la Majaliwa Masepu, mkazi wa Msamvu, alisema: “Sasa hivi ukienda baa au dukani unatakiwa kusema naomba ‘nguruka’, muuzaji atakuuliza unataka nguruka wakubwa au wadogo, maana kuna aina mbili za ujazo wa viroba.” Masepu alisema hatua ya Serikali kuzuia pombe hiyo imeathiri wafanyabiashara na watumiaji kwa kuwa imekuwa ghafla mno kiasi cha kutishia wafanyabiashara wengi kufilisika ikizingatiwa walikuwa na mzigo mkubwa katika maghala yao. “Ni vema Serikali ingetupatia muda hata wa miezi mitatu kumaliza mzigo wetu,” alisema mfanyabiashara mmoja. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urlich Matei, alisema msako huo wa viroba unaendelea na watachukuliwa hatua wafanyabiashara wanaokaidi agizo hilo kwa kuendelea kuuza viroba.
Uhuru kinyatta kuongea na Trump kwa simu.soma zaid
Rais wa Marekani Donald Trump anategemea
kufanya mazungumzo na rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta kwa njia ya simu....
Uhuru Kenyatta atakuwa rais kwanza kutoka
AFRIKA MASHARIKI kuzungumza na rais huyo
kutoka taifa lenye uwezo mkubwa duniani .
Miongoni mwa maswala wanayotarajiwa kugusia
ni swala la usalama ,Somalia na ukame
unaendelea kukumba eneo zima la Afrika
mashariki.
Bosi aliyempa Makonda Hekari 1500 amehojiwa na polisi.soma zaid
Mkurugenzi wa kampuni ya Azimio Housing Estate, Mohamed Ikbal, ambaye hivi karibuni alimgawia ardhi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amehojiwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka za Serikali. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alithibitisha jana kwamba mfanyabiashara huyo aliitwa kwa ajili ya mahojiano, lakini aliachiwa kwa dhamana baada ya muda kuonekana hautoshi. “Alikuja na wakili wake, lakini ameachiwa kwa dhamana ataripoti siku nyingine (hakutaja siku),” alisema Sirro. “Anatuhumiwa kughushi nyaraka za Serikali na sasa upelelezi unaendelea.” Mfanyabiashara huyo inadaiwa kuwa aliripoti polisi jana saa tano asubuhi na kuhojiwa kabla ya kuachiwa kwa dhamana jioni. Kuhojiwa kwa Ikbal, ambaye kampuni yake iliwahi kushirikiana na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika miradi kadhaa tata ya ujenzi, kumekuja siku chache baada ya kumgawia Makonda eneo la ekari 1500 katika kitongoji cha Ligato kijiji cha Kisarawe II wilayani Kigamboni kwa ajili ya viwanda vidogo vidogo. Siku mbili baadaye, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliibuka na kueleza kwamba eneo aliloligawa mfanyabiashara huyo si lake bali linamilikiwa na serikali na wanakijiji. “Eneo lile ni la Serikali si la yule mtu aliyejitangaza anampa Makonda na kwa sababu amemdanganya na mimi ndiye msimamizi wa ardhi, nitamsaidia Makonda kuchukua hatua ili watu wasijipendekeze kusafisha maovu yao kwa kutumia migongo ya viongozi,” alisema Lukuvi. “Hadi siku ile alipokuwa anajipendekeza kwa Makonda, ardhi ile haikuwa yake, wananchi walishashinda kesi mahakamani kwa sababu hakuwa na vielelezo. Ukimdanganya Mkuu wa Mkoa umeidanganya Serikali. Makonda hakuomba ile ardhi ila yeye (Ikbal) ndiye alikwenda kumgawia na amemgawia akijua kwamba alishashindwa kesi,” alisema Lukuvi. Kwa mujibu wa hukumu ya kesi hiyo Na 147 ya mwaka 2015 iliyofunguliwa na Ikbal katika Baraza la Ardhi la Wilaya ya Temeke dhidi ya Baraza la Ardhi la Kijiji, mfanyabiashara huyo alishindwa. “Maombi haya yanatupiliwa mbali pamoja na gharama,” ilisema hukumu hiyo ya Januari 13, 2016. Ijumaa iliyopita mtu aliyejitambulisha kuwa ni mwakilishi wa Ikbal, Kamugisha Katabaro aliibuka na kudai Lukuvi amewasikitisha Watanzania na wataalamu mbalimbali wanaofahamu ukweli wa jambo hilo. Katabaro alidai Ikbal anamiliki ardhi yenye ukubwa wa ekari 3,500 ambayo aliinunua tangu mwaka 2005 kutoka kwa wananchi wa eneo la Lingato. “Wananchi waliliuza hilo eneo bila ya kushurutishwa kwa kufuata taratibu za kisheria na umiliki wa ardhi,” alidai. Mwananchi lilimfuata siku hiyo, Waziri Lukuvi aweke wazi kuhusu mmiliki halali wa eneo hilo naye alisema, “Kama mfanyabiashara huyo anaona ameonewa akate rufaa mahakamani.” Alisisitiza kuwa eneo hilo ni la serikali na watu waliodhulumiwa wameanza kuorodhesha majina yao na wataalamu wa ardhi wapo kwenye eneo hilo wakiendelea na upimaji. “Hiyo ardhi ataipateje wakati mimi ninayo, na kama ana nyaraka zinaonyesha ameshinda mbona hataki kuonyesha anataka kuudanganya umma?” alihoji Lukuvi. Juhudi za kumpata Ikbal hazikuzaa matunda lakini alipoulizwa Katabaro kuhusu mkurugenzi huyo kuitwa polisi alisema ni kweli alitii wito kama alivyotakiwa na polisi. Taarifa kwamba alikamatwa siyo za kweli kwani alihojiwa na kutoka jana jioni baada ya kuwasili kituoni hapo saa tano asubuhi jana,” alieleza. Eneo jingine ambalo Azimio ilizua utata ni umiliki wa ardhi na uthaminishaji wake kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa uitwao Dege Eco Village, Kigamboni. Ulisimama Februari mwaka jana kutokana na utata wa ubia.
TANZIA:Mama wa Rais mstaafu jlJakaya kikwete amefariki dunia.soma zaid
Kupitia ukurasa Instagram wa Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete ameandika ujumbe Kuhusu kifo cha Bi Nuru kama unavyosomeka hapo chini... "TANZIA Ndugu na Marafiki nasikitika kuwatangazia Msiba/Kifo cha Bibi Yetu Bi.Nuru Khalfan Kikwete Kilichotokea asubuhi hii katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa Matibabu. Taratibu za mazishi tutajulishana . Innallilllah wainnaillah rajuun.#"
Vurugu za wamachinga mwanza watu 9 wamejeruhiwa wakiwemo wanamgambo wa jiji.soma zaid
Watu tisa (9) wamejeruhiwa katika vurugu wakati wa kuwaondoa wafanyabiashara wadogowadogo sehemu zisizo ruhusiwa wilayani Nyamagana, mkoani Mwanza Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa w Mwanza DCP Ahmed Msangi imesema kwamba tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.03.2017 majira ya saa15:45hrs katika mtaa wa Buhongwa Center ambapo watu tisa wakiwemo askari mgambo wa jiji la mwanza saba (07), afisa mazingira mmoja (01) na dereva wa jiji mmoja (01) walijeruhiwa. Amesema watu hao walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe sehemu mbalimbali ya miili yao na wafanyabiashara wadogowadogo waliokuwa wakifanya biashara pembeni ya barabara wakishirikiana na watu wengine waliokua wakishabikia wakati wakiendelea na zoezi la kuwaondoa wafanya biashara wadogowadogo katika maeneo yasiyo ruhusiwa haswa kwenye hifadhi ya barabara ya mwanza kwenda shinyanga. Aidha, Msangi amesema katika harakati za kudhibiti vurugu hizo askari walifanikiwa kuwakamata watu tisa ambao inadaiwa kuwa walikuwa wakihusika katika vurugu hizo kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi utakapokamilika, watafikishwa mahakamani. Majeruhi wote wapo hospitali ya mkoa ya Sekou Toure wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao inaendelea vizuri.