Habari ya hivi bunde ccm yakimbilia mahakani kupinga uchaguzi wa meya wa jiji la Dar hapo kesho.soma zaid
CCM wakimbilia mahakamani kuzuia uchaguzi wa
Meya kesho
Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba CCM
wako mahakamani muda huu wakitafuta hati ya
kimahakama kuzuia uchaguzi wa kumpata Meya
wa Jiji la Dar es salaam usifanyike kama
ilivyokuwa imetangazwa hapo awali, na kama
barua za mialiko kwa wajumbe wa kikao hivyo
zinavyoelekeza.
Aidha sababu kubwa inayotajwa CCM kukimbilia
mahamakani kutafuta zuio la uchaguzi wa Meya
wa Jiji inatajwa kuwa ni wao (CCM) kuendelea
kutafuta mbinu ya kushinda uchaguzi huo bila
kujali idadi ya wajumbe wao ni ndogo kuliko ya
Ukawa.
Awali moja ya mbinu tegemeo waliyojua itawapa
ushindi ni kuongeza wabunge wa viti maalum
kutoka nchi jirani ya Zanzibar na wengine kutoka
mikoa ya Tanzania bara, ambao kwa bahati
mbaya baada ya kufuatilia hao wanaotoka mikoa
mingine ilibainika michakato yao ya kusaka
ubunge wa viti maalum ulianzia huko mikoani
kinyume na ukweli kwamba makazi yao yako Dar
es salaam. Na kwa maana hiyo wakaonekana si
wajumbe halali kujumuishwa kwenye uchaguzi
huu.
Kwa wale wabunge wa viti maalum kutoka nchi
jirani ya Zanzibar wao ilibainika kwamba
hawatakiwi kujihusisha na uchaguzi huu wa
kumpata Meya, kwa kuwa wajumbe wote
wataingia kama madiwani na hivyo wao
hawaruhusiwi kwa kuwa suala la madiwani liko
chini ya TAMISEMI, Na suala hilo si la Muungano.
Kwa kuwa mbinu hiyo chafu iliyotaka kutumiwa
na CCM imekwama ,Imekwama, na kwa kuwa
uchaguzi ni kesho tu kama ilivyotangazwa, basi
wameona njia pekee ni kukimbilia mahakamani
tena, kuzuia uchaguzi huo wa kesho usifanyike.
Kwa maoni yangu. Nawaomba CCM wakubali tu
kwamba jiji liko chini ya Ukawa, ni watanzania
hawa, tofauti ni itikadi tu, na kwa kuwa Tanzania
iliridhia kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi
sioni sababu ya msingi kuendelea kulazimisha
wakati mchakato huu ulianzia kwa wananchi
kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwa kuwachagua
madiwani wengi wa ukawa.
Ni bora waachane na figisufigisu hizi za
kulazimisha kuongoza jiji. ...sidhani kama mbinu
hii ya kuendelea kuzuia uchaguzi kwa njia ya
mahakama utawasaidia. ..labda kama wanahitaji
kwenda hatua nyingine mbaya zaidi ya kumwaga
damu ya watanzania kwa kutaka kuongoza jiji,
labda kama wanajipanga kupata umeya kwa
umafia, kwa vurugu na support ya vyombo vya
dola. ...Lakini uchaguzi wa haki na huru, kwa
uchaguzi wa kidemokrasia sioni CCM watashinda
vipi uchaguzi na meya wa Jiji kwa kuwa
uchaguzi ni namba na namba haziongopi.
..Ukawa wana wajumbe takribani 11 zaidi ya
wajumbe wa ccm.
hii ya ccm kukimbilia mahakamani, nawashauri
waachane na mpango huo waache demokrasia
itamalaki.chanzo Dodluck peter mtema .breaking new tz.
0 comments :
Post a Comment