Morogoro sasa kupimwa na kutolewa hati za kimila.soma zaid.
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi
Wiliam Lukuvi ameagiza kupimwa na kutolewa
kwa hati za kimila kwa wananchi wa wilaya ya
Mvomero sambamba na kuheshimiwa na
kutambuliwa kwa hati hizo na taasisi mbalimbali
za kifedha ikiwemo mabenki.
Waziri Lukuvi amesema hayo baada ya kufika
wilayani Kilosa na kupokea taarifa ya usuluhishi
wa migogoro ya ardhi katika kijiji cha Mabwegere
wilayani Kilosa,kazi ambayo awali alimwagiza
aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro
Steven Mashishanga kuifanya,ambapo pia
ametembelea wilaya ya Mvomero akiwa na timu
ya wataalamu wa kuhakiki mipaka ya vijiji sita
vya wilaya hiyo na kupima,ambapo amekuwa ni
waziri wa tatu kutembelea wilaya hiyo ndani ya
kipindi kisichozidi wiki moja,na ametumia fursa
hiyo kuzungumza na baadhi ya makundi ya
wakulima na wafugaji pamoja na viongozi,na
kutoa hati milki za kimila zaidi ya elfu
saba,akitaka zitambuliwe.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr.Rajab Rutengwe
amevitaka vyombo vya usalama kutogeuka
sababu ya migogoro ya ardhi katika wilaya za
mkoa huo,sambamba na kuahidi kubadili viongozi
wa jeshi la polisi hususani wilayani Mvomero ili
kubadili utendaji,ambapo mkuu wa wilaya ya
Mvomero Elizabety Mkwasa akabainisha wapo
baadhi ya wafugaji wanaoshiriki katika kukuza
migogoro wilayani humo ikiwemo kwa kuruhusu
uingizaji wa mifugo kiholela na kutumia watoto
kuchunga bila tahadhari.chanzo itv tz.
0 comments :
Post a Comment