Naibu waziri wa ardh asitisha mkataba na mwenyekit wabaraza la ardhi nyumba na makazi geita.
Naibu waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya
makazi,Angeline Mabula amesitisha mkataba wa
kazi wa Emmanuel Mogasa ambaye Mwenyekiti
wa baraza la ardhi na nyumba la wilaya ya chato
iliyoko mkoani Geita mkoa ili apishe uchunguzi
wa tuhuma zinazochunguzwa juu yake za
kujihusisha na vitendo vya rushwa katika kutoa
maamuzi ya mashauri yanayofikishwa katika
baraza hilo.
Naibu waziri huyo ametoa maamuzi hayo baada
ya kupokea taarifa toka kwa mwenyeti huyo
ambayo ilikuwa inaelezea mwenendo mzima wa
utendaji wa kazi wa baraza hilo.
Amesema amesitisha mkataba wa kazi wa
Mogasa na hivyo atakuwa nje ya ofisi hadi
uchunguzi wa tuhuma zinazomhusu
utakapokamilika na pia ametoa onyo kwa
watendaji idara ya ardhi wa halmashauri ya
wilaya ya chato na kutaka wampe taarifa juu ya
matumizi ya shilingi zaidi milioni 32 zilizotolewa
na wizara kama mkopo kwa ajili ya upimaji wa
viwanja wilayani humo ambao hadi sasa
haurejeshwa wizarani kulingana na makubalino.
Katika hatua nyingine naibu waziri huyo
ameziagiza halmashauri za wilaya na manispaa
kuhakikisha zinatenga viwanja vitakaloliwezesha
shirika la nyumba la taifa kujenga bora kwa
gharama nafuu ili nyumba zinazijengwa
zinazojengwa na ziwe na unafuu kodi, ametoa
agizo hilo baada ya kukagua nyumba zilizojengwa
na shirika hilo wilayani chato na muleba mkoani
kagera.
Naye,Deogratias Batakanwa ambaye ni meneja
wa shirika la nyumba mkoani Kagera na wilaya
ya chato ambayo zamani ilikuwa mkoani humo
kabla ya kuundwa kwa mkoa wa Geita,ameelezea
idadi ya nyumba ambazo shirika hilo limezijenga
mkoani Kagera na wilaya changamoto inayokabili
ujenzi wa nyumba hizo
0 comments :
Post a Comment