Waziri wa awamu ya kikwete atajwa kuwa fisadi ngorongoro.soma zaidi
Ezekiel Maige Atajwa Ufisadi Ngorongoro
Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii katika
serikali ya awamu ya nne, Ezekiel Maige, jana
alitajwa katika kesi inayomkabili aliyekuwa
Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro, Bernard Murunya* ambaye
ameshitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi.
Katika kesi hiyo, Maige anadaiwa kulipiwa nauli
ya safari ya nje na mamlaka hiyo kwa idhini ya
Murunya, ambaye sasa ni Mbunge wa Afrika
Mashariki.*
Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Sezari
Semfukwe, alidai kuwa Murunya na aliyekuwa
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mamlaka
hiyo, Shad Kiambile, waliidhinisha malipo ya dola
66,890. Alidai kuwa fedha hizo zilikuwa kwa ajili
ya safari ya Maige na msaidizi wake aliyetajwa
kwa jina la E. Muyungi na Murunya mwenyewe.
Semfukwe, ambaye ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa
mamlaka hiyo, alidai kuwa Murunya na Kiambile,
ndio walioidhinisha madokezo kwa ajili ya malipo
hayo.*
Akiongozwa na Wakili wa Serikali Hamidu
Sembano, akisaidiana na Rehema Mteta, mbele
ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha,
Patricia Kisinda, Semfukwe alidai kuwa utaratibu
wa maombi ya safari, unatokana na maelekezo
ya mkuu wa idara na kujaza fomu inayoonyesha
anakwenda wapi na kwa muda gani.
Sambamba na hilo, alidai kuwa aina zingine za
safari zinahusisha watu wa nje ambao, si
waajiriwa wa NCAA kwa dokezo la mkuu wa
idara au shirika.
Alidai kuwa alitoa hundi ya malipo namba
309/0238 ya Septemba 9/2011, ambayo ilikuwa
na dokezo la safari kutoka kwa Murunya kwenda
kwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha. Pia *alitoa
hundi ya malipo nyingine iliyokuwa ikionyesha
imelipwa dola zaMarekani *66,890 kwa kampuni
ya Wakala wa Usafirishaji ya Cosmas.
Aliendelea kudai kuwa hundi za malipo namba
310/0379 ya Oktoba 29, 2011 na ankara namba
5609 ya Septemba 7, *2011 zililipwa kwa
Antelope Tours & Traveling kwa ajili ya tiketi za
Murunya, Muyungi na Maige kwa malipo ya dola
za Marekani 66,890 (zaidi ya Sh. milioni 133).
Shahidi hiyo alidai kuwa kumbukumbu ya kitabu
cha malipo ya hundi inaonyesha hundi namba
002758 na 002755 za Septemba 9, *2011
zililipwa kwa kampuni ya Cosmas Travelling
Agent na zilitiwa saini na Kiambile na Murunya.
Hata hivyo, wakati shahidi huyo akitoa vielelezo
hivyo mahakamani hapo ili vitumike kama
ushahidi, malumbano ya kisheria yaliibuka baina
ya mawakili wa pande zote.
Malumbano hayo yaliibuka baada ya upande wa
washtakiwa, ukiongozwa na wakili Amani
Mirambo, kutaka kujua ni vielelezo vingapi au vya
aina gani ambavyo upande wa mashtaka
unavileta.
Hatua hiyo ilisababisha malumbano ya kisheria
hivyo kumfanya hakimu kuahirisha kesi kwa
dakika 10. Baada ya muda huo, alirejea
mahakamani baada ya dakika hizo na kuwahoji.
Baada ya kuhoji pande zote mbili, kutokana na
malumbano ya kisheria, Hakimu alikatizwa na
Wakili wa Serikali Hamidu Simbano,
aliyemwomba *kuahirisha kesi hiyo na kutaja
tarehe nyingine ya *washtakiwa kusomewa
maelezo yao ya awali.
Awali, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),
Rehema Mteta, aliwasomea maelezo ya awali juu
ya tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka
yaliyosababisha mamlaka hiyo kupoteza dola
66,890 (Sh. 133,780,000).
Mteta aliwataja washitakiwa, mbali na Murunya
na Kiambile, kuwa ni Meneja Utalii wa mamlaka
hiyo, Veronica Funguo na Salha Issa ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Cosmas Travelling
Agent.chanzo godluck peter breaking newz tz.
0 comments :
Post a Comment