Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, February 23, 2016

Chama cha CUF kimeitaka tume ya uchaguzi ZEC kutotumia jina alama au picha ya mgombea kutoka cuf.


Chama Cha Wananchi (CUF) kimeitaka Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kuhakikisha haitumii
jina, alama wala picha ya mgombea yeyote wa
chama hicho katika karatasi za kura za uchaguzi
mkuu wa marudio utakaofanyika March 20,
mwaka huu visiwani humo.Akizungumza na
waandishi wa habari mjini hapa jana, Kaimu
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Umma
wa chama hicho, Hamad Masoud, alidai CUF
inatambua kwamba Mwenyekiti wa ZEC, Jecha
Salim Jecha, anatekeleza maagizo ya chama
chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema CUF inawataka wananchi wote wa
Zanzibar, Tanzania na jumuiya ya kimataifa
kutambua kwamba Jecha ametoa taarifa ya
uongo ili kuendeleza upotoshaji alioanzisha kwa
tamko lake la kufuta uchaguzi wa Oktoba 25,
mwaka jana na kuamuru kurudiwa uchaguzi
huo.Alisema CUF haitashiriki katika uchaguzi huo
wa Machi 20, mwaka huu na kuichia CCM
iendelee kujitangazia ushindi wa urais, viti vyote
54 vya uwakilishi na viti vyote 111 vya udiwani.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top