Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, February 23, 2016

Waziri simba chawene aagiza maafisa ardhi na watendaji wanaosababisha migogoro ya ardhi mvomero wafukuzwe kazi.

Waziri wa nchi ofisi ya rais, tawala za mikoa na
serikali za mitaa, Tamisemi, George
Simbachawene ameagiza mamlaka mbalimbali
kuwafukuzwa kazi ndani ya siku 14 watendaji na
wenyeviti wa vijiji watakaobainika kuhusika na
uchochezi wa migogoro ya ardhi wilayani
Mvomero, sambamba na kuhamishwa kwa
watumishi waliokaa muda mrefu katika wilaya
hiyo.
Waziri Simbachawene amesema hayo wakati
akizungumza na viongozi na watumishi wa
halmashauri ya wilaya ya Mvomero na mkoa wa
Morogoro, ambapo amepokea taarifa
inayohusiana na changamoto za wilaya hiyo
ikiwemo juu ya migogoro ya ardhi, huku lawama
zikielekezwa na viongozi kwa baadhi ya
watendaji na viongozi wa serikali katika kuhusika
na kukuza na kuendeleza migogoro hiyo pamoja
na ukosefu wa baraza la ardhi katika wilaya hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dr Rajab Rutengwe
katika kikao hicho, ameiomba mamlaka ya kuzuia
na kupambana na rushwa Takukuru kuwaongeza
wataalamu ili kukabiliana na maswala ya rushwa
ambayo yameonekana kushika kasi katika baadhi
ya wilaya na kusababisha migogoro ya ardhi
kuzidi kukua, ambapo waziri Simbachawene
akaagiza kuchunguzwa na kufukuzwa kwa
watendaji wote watakaobainika kuchangia kukua
kwa migogoro hiyo ya ardhi na kwamba serikali
haitamvumilia yeyote atakayebainika kuwa
chanzo cha migogoro hiyo.
Katika siku ya pili ziara yake mkoani Morogoro,
waziri huyo wa Tamisemi ameweza kuembelea
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na
kueleza kuridhishwa na utendaji kazi na jitihada
zinazofanywa na watumishi, wakiongozwa na
mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dk Ritta
Lyamuya, pamoja na kukagua mradi wa ujenzi wa
kisasa wa kituo kikuu cha mabasi Msamvu,
pamoja na kuzungumza na viongozi wa mkoa,
wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri
za wilaya.chanzo Itv.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top