TAMISENI yawataka watumishi mkoan Arusha kutofanya kazi kwa mazoea.soma zaidi.
Tamisemi yawataka watendaji mkoani Arusha
kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Naibu waziri wa Tamisemi Bw.Suleimani Jaffo
amemtaka katibu tawala wa mkoa wa Arusha
kumpatia orodha ya watendaji wanaoendelea
kufanya kazi kwa mazoea na kusababisha
wananchi kuteseka bila sababu za msingi ili
hatua zikiwemo za kuwafukuza kazi zichukuliwe
haraka kwani wakati wa kubembelezana
umekwisha.
Mh.Jaffo ameyasema hayo baada ya kupewa
taarifa inayopingana na hali halisi ya utekelezaji
wa majukumu mbalimbali likiwemo la
kushughulikia maafa yanayowapata wananchi
iliyosababisha baadhi ya watendaji kushindwa
kujieleza na wengine kutupiana lawama na
kuikana maelezo yao wenyewe.
Mkanganyiko wa watendaji hao ulikuja baada ya
naibu waziri Mh.Jaffo kutaka kupata maelezo ya
watendaji hao wanavyoshughulikia majanga
mbalimbali yanayowapata wananchi likiwemo la
kuezuliwa kwa shule ya msingi isimani lililotokea
Desemba mwaka jana ambalo hadi sasa hatua
hazijachukuliwa licha ya kuwa ndani ya uwezo.
Katika sakata hilo kadiri viongozi na watendaji
hao walivyojaribu kutoa maelezo yaliendelea
kutofautiana jambo ambalo Mh.Waziri.Jaffo
amesema linalodhihirisha wazi kuwa lipo tatizo
ambalo serikali haiwezi kuendelea kulifumbiwa
macho.
Mh.Naibu waziri Suleiman Jaffo alifanya ziara ya
kushtukiza mkoani Arusha ambayo inadaiwa
kuwa ni matokeo ya malalamiko ya wannachi
wakiwemo wanaopatwa na maafa ama majanga
mbali mbali ya kuchelewa kupata msaada wa
serikali licha ya kupewa ahadi kila janga
linapotokea.
wana mkomoa lema na chadema.
0 comments :
Post a Comment