Miundombinu ya muwekezaji wa shamba la TPC kilimanjaro rahalibiwa na wananchi.soma zaidi.
Wakulima wa mpunga katika skimu ya
umwagiliaji Mawala kata ya Kahe wilaya ya
Moshi mkoani Kilimanjaro wamevamia na
kuharibu miundombinu ya ugawaji maji kupeleka
katika mashamba ya miwa ya mwekezaji wa
kiwanda cha sukari TPC.
Wakulima hao wamesema wamelazimika kufanya
uharibifu huo na kuelekeza maji katika mfereji wa
mashamba ya wakulima kwa madai ya
mwekezaji huyo kukausha maji yote mferejini na
kuelekeza kwenye mashamba ya miwa hali
ambayo imesababisha kusababisha mpunga
uliopandwa kukauka kwa kukosa maji.
Wamesema wanasikitishwa na hatua ya
mwekezaji huyo kukiuka makubaliano ya
kugawana maji hayo kwa wiki siku tatu badala
yake anatumia mashine ya kuvuta maji yote
mferejini na kueleleza kwenye mashamba ya
miwa hali ambayo imesababisha mashamba ya
mpunga kukauka kwa kukosa maji.
Diwani wa kata ya Kahe mashariki Bw. Rodrick
Mmanyi amelazimika kufika katika eneo la tukio
na kuwataka wakulima kuacha kufanya vurugu na
kuahidi kushirikiana na viongozi wa umoja wa
wakulima hao ili kufanya mazungumzo na
uongozi wa kiwanda cha sukari TPC kumaliza
mgogoro huo ambao unahatarisha amani.
Hata hivyo juhudi za kumpata afisa utawala wa
kiwanda cha sukari TPC Japhary Ally
kuzungumzia mgogoro huo hazikufanikiwa baada
ya kusema yuko kwenye kikao ambapo kamanda
wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Ramadhani Mungi
amesema amepata taarifa hizo na kwamba yuko
safarini atatoa taarifa hizo kesho.chanzo ITV TZ.
0 comments :
Post a Comment