Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, February 21, 2016

Tatizo la afya nchini bado ni changamoto kitanda kimoja walala watu 2.sma zaid.

Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete
iliyoanzishwa mwaka 1906, inakabiliwa na
changamoto ya akinamama wazazi na
wanaojifungua kulala zaidi ya wawili katika
kitanda kimoja, hali ambayo imedaiwa kuwa,
naweza kusababishia watoto wanaozaliwa
kuondoka na maambukizi katika kile
kinachodaiwa kuwa ni miundomninu ya zamani
ya majengo kutofanyiwa marekebisho.
Hayo yamebainishwa na katibu tawala msaidizi
huduma za afya mkoa wa Tabora ambaye pia ni
mganga mkuu wa mkoa Dkt Gunini Kamba,
wakati akitoa taarifa kwa mbunge wa viti maalum
Chadema aliyekwenda hospitalini hapo kwa lengo
la kutambua changamoto na kutafuta ni jinsi gani
anaweza kushiriki katika kuzitatua.
Kwa upande wake mbunge huyo wa viti maalum
mkoa wa Tabora Chadema Mhe. Hawa
Mwaifunga amesema kuwa, kwa pamoja
wabunge kumi na nne wa mkoa wa Tabora kila
mmoja akitoa sehemu ya kipato kinachotokana
na nafasi zao, wanaweza kutatua changamoto
hizo na kuisaidia serikali kutekeleza majukumu
yake.chanzo radio one stereo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top