Wauza simu waomba waonzewe mda wa kuzima simu feki..soma zaidi.
Wakati tarehe kumi na saba juni mwaka huu simu
zote feki zikitarajiwa kuzimwa baadhi ya
wafanyabiashara za simu za mikononi katika
soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam walalamikia
kukosa kabisa wateja na kupata hasara kubwa
kutokana na kuwa na simu nyingi ambazo ni feki
huku watuamiaji nao wakilalamikia kuwa
watakosa mawasiliano kutokana na simu origino
kuwa ghali.
Siku chache baada ya mamalaka ya mawasiliano
nchini TCRA kuonesha msimamo wake wa
kuzifungia simu hizo baadhi ya wafanyabiashara
katika soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam
wameelezea kuwa katika wakati mgumu
kutokana na kukosa wateja na hivyo kusababisha
hata simu ambazo sio feki kukosa wateja na
kubaini kupata hasara kubwa kutokana na azimio
hilo ambapo wameziomba mamlaka husika
kuongeza muda ili kuwapa nafasi ya kujipanga ili
kutafuta mtaji wa kuingiza simu zinazotakiwa.
Baadhi ya watumiaji waliozungumza na ITV nao
wameitupia lawama serikali kwa kutoa agizo la
kuzimwa kwa simu feki huku ikiruhusu simu hizo
kuingia nchini na kuzitaka mamlaka husika
kulitizama upya swala hilo ama kuweka bei
elekezi kwa simu halisi ili iwe rahisi kwa
wananchi wa kipato cha chini kuzinunua.
Wapo baadhi ya wauzaji wa simu pia
walioipongeza serikali kwa hatua iliyochukuwa ya
kuzima simu feki na walikuwa na haya ya
kusema.
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA tayri
imeonesha msimamo na kutangaza kuwa tarehe
kumi na saba juni mwaka huu simu zote feki
zitazimwa ikumbukwe kuwa zoezi la kufungiwa
kwa simu feki sio geni kwa nchi za Afrika
Mashariki ikiwemo Kenya ambao tayari
wameshazifungia kabisa simu feki.
0 comments :
Post a Comment