Trump aibuka mshindi south carolina.soma zaid.
Mgombea kiti wa chama cha Republican katika
uchaguzi ujao wa urais nchini Marekani Donald
Trump ameshinda kura ya mashinani katika
jimbo la Carolina Kusini.
Bwana Trump ambaye awali mwezi huu,
alishinda katika jimbo la New Hampshire,
amepata kura nyingi huko Carolina Kusini huku
wapinzani wake Ted Cruz na Marco Rubio
wakimfuatia kwa karibu.
Kutokana na matokeo mabaya ya gavana wa
zamani wa Florida, Jeb Bush, kakake aliyekuwa
Rais wa Marekani George W. Bush, amejiondoa
katika kinyanganyiro hicho.
Awali mgombea kiti hicho kwa chama cha
Democrats Bi Hillary Clinton ameibuka mshindi
katika kura ya mashinani eneo la Nevada, na
kubwaga mpinzani wake Bernie Sanders.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako.
0 comments :
Post a Comment