January 21, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, February 20, 2016

Msimamo wa Cuf zanzibar waendelea.

Mshindo wa CUF Z’bar
KIMYA cha viongozi wa Chama cha Wananchi
(CUF) kina mshindo visiwani Zanzibar, hata hivyo
chama hicho kinasema kinapambana na sera za
kibabe za Serikali ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM),
Kinaeleza kuwa, umoja na mshikamano wa
wapenda haki hasa katika kipindi hiki cha
mgogoro wa kisiasa ndio njia pekee ya
kuhakikisha sera haramu na za kibabe zinazikwa
visiwani humo.
Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa Mipango,
Uchaguzi ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu Taifa
amesema, CUF na Watanzania sasa wanaelewa
kwamba, kwa Serikali ya CCM hoja si haki
isipokuwa kupata kile wanachokitaka.
Akizungumza na mtandao huu leo kwenye Ofisi
Kuu ya CUF amesema, CCM haifuati sheria na
imejikita katika kukandamiza uhuru na
demokrasia huku utafutaji wa suluhu ukiwa ni wa
mabavu.
“Mambo mengi yanayofanywa na serikali
hayafuati sheria na misingi ya demokrasia,
hufanya mambo kwa kulinda maslahi ya chama
tawala hata kama wanajua wanavunja sheria,”
amesema Mketo.
Ametaja baadhi ya mambo ambayo yanaviashiria
vya uvunjwaji wa sheria na ukandamizaji wa
demokrasia kuwa ni pamoja na kulazimisha
vyama vya siasa kufuata matakwa yao pia Jeshi
la Polisi kutotendea haki vyama vya upinzani.
“Kufutwa na kurudiwa kwa uchaguzi visiwani
Zanzibar bila ya sababu za msingi ni
kuikandamiza demokrasia na kukiuka sheria,
kama uchaguzi haukuwa wa haki, nani
aliyeipoteza haki?” amehoji Mketo na kuongeza;
“Hata siku moja chama cha upinzani
hakitafanikiwa kuiba kura, sababu Tume na
watendaji wake huchaguliwa na Rais ambaye
anatoka chama tawala.
“Ili wapinzani waibe kura inabidi washirikiane na
Tume ambao ni Mwenyekiti, Wakurugenzi na
Makamishina, wote wamechaguliwa na Rais, kwa
hiyo si rahisi kuwarubuni,” amesema.
Mketo amedai kuwa, chaguzi nyingi zilizopita
mgombea wa CUF alikuwa ni mshindi lakini
waliminya demokrasia kwa Tume kumpitisha
wanayemtaka, pia ametoa mfano wa uchaguzi
uliofanyika mwaka 1995.
“Uchaguzi wa mwaka 1995, mgombea wa
upinzani alipita, kituo cha televisheni cha DTV
ambacho sasa ni Chanel Ten, kilifungiwa baada
ya kutangaza kuwa Maalim Seif aongoza
Zanzibar,” amesema.
Mketo amesema, wagombea wote wa CUF
wameiandikia barua tume ya ZEC na viapo ili
kuwaeleza kwamba, hawatashiriki katika
uchaguzi wa marudio.
“Hata kama ZEC ikilazimisha kuweka jina la
Maalim Seif Shariff Hamad wa CUF na
ikaonekana ameshinda, Maalim Seif hatokubali
kuichukua nchi, sababu ameshakataa kurudiwa
kwa uchaguzi,” amesema na kuongeza;
“Wananchi wengi wa Zanzibar hawakubali
kurudia uchaguzi, wanaijua demokrasi na haki
yao, hawatapiga kura sababu viongozi
wanaowataka, wameshawachagua.”
Kuhusu kuzuiliwa kwa maandamano ya Jumuiya
ya Wanawake CUF-Taifa amesema, kitendo cha
polisi kuwanyima kibali ni kinyume cha sheria na
walikifanya hivyo ili kulinda masilahi ya serikali.
“Kwa mujibu wa sheria namba 5 ya vyama vya
siasa ya 1992, imetoa haki kwa vyama vya siasa
kuandamana na inasema vyama vinatakiwa kutoa
taarifa ya maandamano kabla ya siku mbili,”
amesema Mketo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top