Al Qaida wateka mji wa Ahwar,Yemeni.
Inaarifiwa kuwa wapiganaji kadha wa al-Qaeda
nchini Yemen, wameuteka mji wa Ahwar, Kusini
mwa Yemen.
Duru za huko zinanukuliwa kusema kwamba,
wakati wapiganaji walipoingia mjini humo,
walipambana na kikosi kilichokuwa kikilinda mji
huo na watatu waliuwawa.
Vilevile wapiganaji waliweka vizuizi vya
barabarani na kupandisha bendera yao katika
majengo ya serikali.
Wadadisi wanasema, kwa kuteka mji wa Ahwar,
itaisaidia al-Qaeda kujizatiti katika mwambao wa
jimbo la Abyan, ambako tayari inadhibiti miji
mengine miwili.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako
0 comments :
Post a Comment