Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, February 20, 2016

Oparation ya utumbuaji majibu kwa wasio lipa kodi sio uonevu.asema waziri mkuu.

Waziri Mkuu Mheshimiwa KASSIM MAJALIWA
amesema oparesheni ambayo inafanyika sasa
kuhakikisha kila mtu analipa kodi na kudumisha
nidhamu kwa watumishi wa umma haina nia ya
kuwaadhibu watu.
Amesema hatua hiyo ni kuhakikisha kila mtu
anatekeleza wajibu wake wa kulipa kodi ili
serikali iweze kutekeleza mipango yake
iliyojiwekea na hivyo amewaomba wananchi
kuisaidia serikali kutekeleza oparesheni hiyo.
Mheshimiwa MAJALIWA ameyasema hayo katika
mkutano wa Jumuiya ya Wanarukwa na Katavi
waishio jijini Dar es Salaam ambapo amesema
serikali haitamuonea mtu wala huruma mtu
yoyote ambaye anakwenda kinyume na sheria za
nchi.
Aidha mkuu huyo amewataka Watanzania
kutumia fursa zinazowazunguka kama madini,
kilimo, mifugo na nyingine za kujiletea
maendeleo.
Naye Waziri Mkuu Mstahafu MIZENGO PINDA
amesema kwa sasa kila mtu anapaswa kujua
kuwa ni jukumu lake kujiletea maendeleo kwani
haitakuwa na faida yoyote kama mtu amebaki
kuikosoa serikali bila ya kutoa njia mbayala ya
kurekebisha hicho ambacho anaona hakijawa
sawa.chanzo itv tz.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top