Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, February 18, 2016

Uturuki yaapa kulipiza kisasi shambulio.

Uturuki imeapa kulipiza kisasi dhidi ya
washambuliaji wa mlipuko mkubwa wa bomu
katika mji mkuu wa Ankara,ambao umewawacha
watu 28 wakiwa wamefariki na wengine 61
wakijeruhiwa.
''Uturuki haitaogopa kutumia uwezo wake wa
kujilinda,rais Recep Tayyip Erdogan amesema.
Maafisa wamesema kuwa gari lililojaa vilipuzi
lililipuliwa wakati ambapo mabasi ya jeshi
yalikuwa yakipita siku ya jumatano.Mazishi
yanatarajiwa kufanyika siku ya Alamisi.
Hakuna kundi lolote kufikia sasa lililodai
kutekeleza shambulio hilo.
Marekani ilishtumu mlipuko huo ,huku msemaji
wa baraza la usalama wa kitaifa Ned Price
akisema,tunasimama pamoja na Uturuki ,mshirika
wa Nato na mshirika wetu mkuu.
Mlipuko huo ulitokea katika eneo la karibu na
bunge na makao makuu ya jeshi.
Moshi mkubwa ulionekana ukifuka kutoka eneo
hilo na mashahidi wanasema mlipuko huo
ulisikika mji mzima.chanzo bbc.com.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top