Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, February 18, 2016

Wakazi 150 gongolamboto walazimika kulala inje baada ya nyumba kubomolewa.soma zaidi.

Wakazi zaidi 150 wa Guluka kwalala
Gongolamboto jijini Dar es Salaam ambao
nyumba zao 25 zimebolewa wamesema kwa sasa
watalazimika kulala nje kwa kukosa nyumba za
kuishi baada ya zoezo la bomoabomoa kufanywa
na uongozi wa kiwanda cha kampuni ya NAMERA
huku wakazi hao wakisema zoezi zima la
ubomoaji limefanyika wakati kesi kuendelea
kusikilizwa katika mahakama ya ardhi.
Wakiongea na ITV mara baada ya kufika katika
eneo hilo la Guluka kwalala na kushuhudia
mabaki ya nyumba ambazo zimebomolewa
wananchi hao wamelalamikia zoezi zima la
ubomoaji wa nyumba hizo baada ya idadi kubwa
ya wakazo hao kushindwa kutoa samani zao
ndani wakati zoezi la ubomoaji likifanyika na
kusimamiwa na askari wa jeshi la polisi.
Bwana Fitiri Juma ambaye ni mjumbe wa seikali
ya mtaa wa Guluka Kwalala akiongea na ITV
amelalamikia viongozi wote wa eneo hilo kutofika
wakati zoezi la ubomoaji likendelea na
kusababisha wananchi hao kupata hasara ya mali
zao.
Katika kutaka kujua juu ya uhalali wa zoezi zima
la ubomoaji kama limezingatia misingi ya sheria
ITV iliutafuta uongozi wa kiwanda cha NAMERA
ambapo uongozi umekiri kutelezela zoezi hilo na
kulipa fidia wananchi wote waliojenga eneo hilo
wanalodai ni la kiwanda.chanzo itv.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top