Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, February 18, 2016

Kwa mara ya kwanza tangue aingie madarakani.Rais azungumza na wasanii.

Rais Magufuli akiambatana na makamu wa Rais
Mh. Samia Suluhu Hassani, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi
Abdalah Bulembo pamoja na mawaziri kadhaa wa
serikali yake amekutana na makundi hayo ikulu
jijini Dar es salaam kwa nia ya kuwashukuru na
kutoa agizo la katazo la utoaji wa vibali vya
kuagiza sukari kutoka nje ya nchi.
Aidha Dkt Magufuli ameiagiza mamlaka ya
mapato Tanzania (TRA) kufanya operesheni
maalum ya kukamata kazi zote za wasanii zisizo
na alama maalum ya mamlaka ya mapato nchini
kufuatia malalamiko ya wasanii kushindwa
kumudu ushindani katika soko kutokana na kazi
nyingi kuingizwa nchini bila ya kulipia ushuru.
Pia amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni
Sanaa Na Michezo Mh. Nape Nnauye kuangalia
utaratibu wa chama cha haki miliki Tanzania
(COSOTA) kuwa chini ya wizara yake tofauti na
ilivyo sasa ambapo chama hicho kiko chini ya
wizara ya viwanda na biashara.
Kwa upande wake makamu wa Rais Mh. Samia
Suluhu hassani amewashukuru wasanii hao kwa
mchango wao uliokiwezesha Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kushinda uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015 na kuwataka kuendelea kushirikiana
na serikali katika masuala mbalimbali ya
kuhamasisha maendeleo huku waziri mkuu Mh
Kassim Majaliwa akiwaahidi kusimamia kwa
vitendo maagizo yote yaliyotolewa na Rais.
Kwa upande wasanii hao wamemshukuru Rais
kwa uamuzi wake wa kuwaita na kuzungumza
nao ikiwa ni jitihada za kutambua mchango wao
katika uchumi na maendeleo ya nchi na miongoni
mwa makundi yaliyofanikisha chama cha
mapinduzi kushinda katika uchaguzi mkuu wa
2015..

0 comments :

Post a Comment

Back To Top