Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, March 24, 2016

BASATA yapiga marufuku Disko toto.soma zaidi.

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa
na burudani nchini linawakumbusha
wamiliki na waendeshaji wa kumbi za
burudani kufuata sheria, kanuni na
taratibu walizopewa kwenye vibali vyao
vya uendeshaji wa kumbi.
Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na
vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao,
kuzingatia muda wa utumizi wa kumbi,
kuepuka kelele zinazosumbua kwenye
maeneo maalum hasa makazi ya watu na
kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha
ya watu na mali zao.
Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki
wote wa kumbi za sherehe na burudani
kwamba ni marufuku kukusanya watoto
katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa
‘Disko Toto’ katika msimu huu wa
Sikukuu ya Pasaka ili kuepuka maafa
yanayoweza kujitokeza.
Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za
sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi
wamekuwa wakijisahau na kuendekeza
faida katika biashara zao kiasi cha
kuandaa madisko ya watoto hali mbayo
imekuwa ikisababisha maafa ambayo
yangeepukika kwa kufuata sheria, kanuni
na taratibu.
Aidha, baadhi ya wamiliki na waendeshaji
wa kumbi kwa msingi huohuo wa
kuendekeza faida pasi na kujali
maelekezo ya vibali vyao wamekuwa
wakijaza watu kupita viwango vya
madaraja waliyopangiwa na BASATA.
BASATA kama mtoaji wa vibali vya kumbi
za sherehe na burudani linasisistiza
kwamba halitafumbia macho ukumbi
wowote utakaokiuka maelekezo haya
sambamba na kuruhusu maonesho
machafu yenye kudhalilisha utu wa
binadamu hasa yale yanayoonesha
maungo ya ndani. Hatua kali na za
kisheria zitachukuliwa kwa yeyote
atakayekiuka maagizo haya.
BASATA linawatakia wasanii na wadau
wote wa Sanaa Pasaka njema na yenye
furaha tele.
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA
KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA

0 comments :

Post a Comment

Back To Top