Halmashauli ya Bariadi mkoani simiyu imewasimamisha watumishi watatu
Serikali wilayani Bariadi Mkoani Simiyu
imewasimamisha kazi Watumishi watatu wa
Halmashauri ya Bariadi kwa tuhuma mbalimbali
ikiwemo ya walimu kuuziwa vitambulisho vya
kazi,fomu ya (OPRAS) na walimu 22
waliosimamishwa na kurudishwa kazini na
kushindwa kulipwa madai yao ya miaka mitatu
kiasi cha milioni 150 baada ya kuagizwa na Tume
ya walimu TSD na kukaidi kufanya hivyo.
Uamuzi wa kuwasimamisha kazi Watumishi hao
umekuja muda mfupi baada ya kumalizika kwa
kikao cha pamoja kati ya Mkuu wa Wilaya hiyo
Ponsiano Nyami na waalimu zaidi ya elfu moja
wa Wilaya ya Bariadi kilichofanyika katika Ukumbi
wa Bariadi Motel ambapo walipomueleza mkuu
huyo namna wanavyonyanyasika na watumishi
hao kiasi cha kukata tamaa,ya kufundisha
kutokana na madai yao yakiwemo malimbikizo ya
mishahara.
Mara baada ya kikao hicho Mkuu wa Wilaya
akaitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Ulinzi
na Usalama,ambapo akatoa kauli ya Serikali ya
kuwasiamamisha Watumishi hao mbele ya
waandishi wa habari.
Sambamba na kuwasimamisha Watumishi hao pia
ameviagiza Vyombo Dola ikiwemo Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU
kuhakikisha wanachunguza tuhuma zote
zinazowakabili,huku akimuagiza Mkuu wa Polisi
wa Wilaya kuwakamata na kuwafikisha
ahakamani wale wenye maduka ya vifaa vya
shule ambao wamekuwa wakiuza za fomu za
OPRAS ambazo ni za serikali katika maduka yao
0 comments :
Post a Comment