Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, March 30, 2016

Hali ya joto Inayaonzengeza hapa nchini yasababisha ndoa nyingi kutetereka ''nani kasema" ? soma zaid.

Kutokana na hali ya joto iliyopo jijini Dar es
Salaam, Askofu wa Huduma ya Good News for
All, Charles Gadi amefanya maombi kuomba
mvua katika ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo
mara baada ya kuzungumza na waandishi wa
habari.
Maombi hayo yaliyofanyika kwa nusu saa,
yaliwashirikisha waandishi wa habari na
wachungaji mbalimbali wa huduma hiyo. Katika
maombi hayo yaliyofanyika jana, jijini humo,
Askofu Gadi alisema hali ya hewa imekuwa ya
joto kubwa kama ilivyotangazwa na Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Alisema hali hiyo imesababisha familia na ndoa
kukosa raha na kushindwa kuzaliana kama
ilivyoelezwa katika Biblia kwamba wazae waijaze
dunia.
‘’Wanandoa wanakosa raha, watu wanalala nje
kwa sababu ya joto kali lililokuwepo. Mwaka jana
katika kipindi hiki cha Pasaka kulikuwa na mvua
kubwa zilizosababisha mafuriko lakini ni tofauti
na mwaka huu, hivyo tuombee mvua,’’ alisema.
Alisema inapaswa kuendelea kuomba ili watu
waweze kuishi kwa amani na kwamba endapo
watu hawataomba, inawezekana kusiwe na mvua
za masika kama walivyozoea.
Askofu Gadi aliongeza kuwa ni lazima kuomba ili
kuwe na mvua za kutosha nchi iweze
kujitegemea kwa chakula kwa muda wote wa
utawala wa Rais Dk John Magufuli.
‘’Tuombe ili fedha ambazo Rais Magufuli
angetakiwa kuzitumia kwa ajili ya kuagiza
vyakula, zitumike kwenye kuleta maendeleo
mengine ya muhimu kwa Taifa letu. Pia itasaidia
kuimarika kwa mbuga za wanyama katika
kuendeleza na kuinua sekta ya utalii nchini,’’
alifafanua Askofu Gadi.chanzo time fm.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top