Askari kikosi za zimamoto wanusurika kuchapwa kipigo kutoka kwa wananchi mkoani shinyanga.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto, Manispaa ya
Shinyanga wamenusurika kipigo kutoka kwa
wananchi wa mtaa wa Banduka, kata ya Ndala
mjini hapa, baada ya kuchelewa kufika kwenye
tukio la nyumba kuungua moto ikiwa na watoto
ndani yake.
Baadhi ya mashuhuda walidai kuwa moto huo
ulianza kuwaka kwenye nyumba ya Azizi
Abdallah, saa 2:00 asubuhi na uliunguza baadhi
ya vitu kwenye nyumba hiyo ambayo wanaishi
wapangaji pekee kwa kile kinachosadikiwa kuwa
ni hitilafu ya umeme ambayo imekuwa ikijitokeza
mara kwa mara.Mmoja wa walioshuhudia,
Onesmo Shija, alisema wapangaji wote walikuwa
wamekwenda makazini na kubaki watoto ambapo
saa 2:00 aliona moshi ukifuka kwenye madirisha
huku watoto wakipiga kelele, ndipo
walipokusanyika na kuanza kuuzima na
kuwanusuru kifo watoto hao.Shija alisema baada
ya wananchi kutoa taarifa mapema kwa kikosi
hicho, walichelewa kufika na walipofika tayari
moto ulikuwa umeshazimwa ndipo wananchi
walipopandwa hasira na kuanza kuokota mawe
na kuwashambulia lakini mwenyekiti wa mtaa
aliwazuia.Mwenyekiti wa mtaa huo, Terege
Nyankangara alisikitishwa na kikosi cha
Zimamoto kuchelewa kufika eneo la tukio na
kueleza uchelewaji huo ulitaka kuhatarisha
amani. Hata hivyo, Nyankangara aliwaasa
wananchi wake kuacha tabia ya kujichukulia
sheria mkononi.
0 comments :
Post a Comment