Kama unania ya kuwa mkulima ya kilimo cha mapapi soma hii itakusaidia.
SOMA HII INAWEZA KUKUSAIDIA KATIKA
KUFIKIA MALENGO YAKO
HEBU CHUKUA KALUKUKETA YAKO, TUFANYE
HESABU..!!
Eka moja ya shamba la papai inaweza kuingiza
miche 1000-1200(elfu moja hadi elfu na mia
mbili)-zile mbegu fupi. Tufanye umepanda miche
1,000. Mti mmoja ukiuhudumia vema unaweza
kutoa matunda hadi 120 kwa msimu. Tufanye
umetoa matunda 80, tu. Tunda moja kwa bei ya
shamba tufanye umeuza bei ya "kutupwa" ya
Tsh. 500/= (lakini papai lililoshiba linauzwa hadi
Tsh. 3,000/= sokoni). Chukua 500/= mara 80
unapata 40,000/=(elfu arobaini kwa mti mmoja).
Sasa chukua 40,000/= zidisha mara 1,000
unapata 40,000,000/=(milioni arobaini). Gharama
za kulima papai ekari moja haizidi milioni mbili.
Toka kupandwa hadi kuvunwa papai inachukua
miezi kumi tu. Tufanye hivi: ukishavuna hii
milioni 40 jibane, usiitumie, mwaka unaofuata
nenda kapande tena papai ekari 20! Kama
kalukuketa yako haisumbui utapata total ya Tsh.
Milioni mia nane (800,000,000/=). Hapo
nakuruhusu chukua milioni 100 zitumbue kwa
raha zako(na mtu yeyote akikuhoji kwa nini
unatumbua pesa nyingi namna hiyo? Mwambie
Sanga kaniruhusu!), Then, milioni 200 wekeza
tena shambani, halafu milioni 500 weka benki.
Naishia hapa kuhusu "kukalukuketi", malizia
mwenyewe uone kama utakosa milioni 890 ndani
ya miaka mitano. Tuache hayo. Najua utaniuliza,
maswali kuhusu soko, hali ya hewa, udongo,
mbegu na mengine. Tafadhali hayo maswali
tafuta majibu mwenyewe, (nimekuachia home
work-usilete uvivu wa kutafuniwa kila kitu).
Lakini ukilima mapapai ukakosa soko hapa nchini
kuna nchi nahitaji sana kama vile Comoro na
Madagascar. Kama umeungana na waliokariri
kwamba hela ni ngumu zama hizi za mtumbua
majipu, shauri yako, maana huo sasa ni uzembe
laivu!
Kwa haya na mengine mengi usisahau Ku like
page hii.
Sunday at 3:31am · Public · in Tim
0 comments :
Post a Comment