Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, March 29, 2016

Madudu tena yagunduliwa PTA(bandarini).soma zaidi.

Wajumbe wa Kamati hiyo, mbunge wa Mbeya
Vijijini Bw. Oran Njeza pamoja na mwenzake wa
Tunduma wamesema taarifa ya fedha ya
mamlaka hiyo inaonesha uwepo wa mapungufu
makubwa ambayo yasiporekebishwa, mchango
wa sekta ya bandari katika uchumi utaendelea
kudidimia siku hadi siku.
Aidha, mbunge wa Mtwara Mjini Bw. Maftah
Abdallah Nachuma amehoji, dhana ya mradi wa
ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo, wakati
ambapo mamlaka hiyo imekuwa ikihaha kutafuta
pesa kwa ajili ya kuboresha bandari zake
ikiwemo ya Mtwara ambayo inahitaji ukarabati
mkubwa chini ya mradi wa ukanda wa kiuchumi
wa Mtwara.
Kwa upande wake, Mbunge wa Bunda Mjini Bi.
Easter Bulaya amehoji ni kwanini TPA imekuwa
haishughulikii tatizo la bandari bubu zilizozagaa
maeneo mengi ya ukanda wa bahari ya Hindi,
hasa katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam,
huku mizigo inayopitia katika bandari ya Dar es
Salaam ikiwa inapungua.chanzo east africa television.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top