Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, March 29, 2016

Hivi nchi hii ya tanzania ni masikini kama mtumishi wa umma analipwa mshahara million 40 kwa mwezi?

Rais wa Tanzania John Magufuli ameahidi
kwamba kuanzia bajeti ijayo kodi katika
mishahara kwa wafanyakazi itapungua kutoka
asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9.
Aidha, pis alisema ataweka kiwango cha kima cha
juu na kwamba wale wote wanaopokea
mishahara ya hadi shilingi milioni 40, itapunguwa
na haitazidi milioni 15
Rais Magufuli aliyasema  hayo hapo jana alipokuwa
akizungumza katika mkutano wa hadhara
Kaskazini Magharibi mwa Tanzania (Wilaya ya
Chato, Mkoa wa Geita) ambapo aliwataka
wananchi wafanye kazi kwa bidii ili kuondokana
na tabia ya utegemezi wa misaada ya nje.
Magufuli apiga simu kituo cha runinga
"Ni lazima tujisimamie sisi wenyewe. Na
tukijisimamia sisi wenyewe kwa kila mmoja
kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi
afanye kazi kwelikweli. Kama ni mkulima afanye
ukulima kweli kweli, kama ni mfanyabiashara
afanye biashara kweli kweli, kama ni mfugaji
afuge kweli kweli, kama ki mvuvi avue kweli
kweli, Tanzania hii tutavuka," amesema Magufuli.
Awali, Dkt Magufuli, aliagiza kufunguliwa kwa
barabara ya Uwanja wa Ndege Mwanza-Igombe
hadi Kayenze yenye urefu wa kilomita 7.
Barabara hiyo ilifungwa kupisha upanuzi wa
uwanja huo tangu mwaka 2014.
"Nafahamu suala linalowaumiza wananchi la
kufungwa kwa barabara ya Airport-Igombe yenye
urefu wa kilomita 7, sasa naagiza kuanzia sasa
kufunguliwa kwa barabara hiyo ili wananchi
watumie kupita ili kuondoa usumbufu wa
kuzunguka kule maeneo ya Nyakato hadi maeneo
ya TX Kata ya Bugogwa, Kata ya
Sangabuye,”alisema.chanzo(BBC).

0 comments :

Post a Comment

Back To Top