Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, March 29, 2016

Rais magufuli atua kwao chato kwa kishindo na kuongea yafuatayo.sima zaidi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
wananchi wa Chato mara baada ya kumaliza
kuwahutubia katika mkutano wa hadhara jana
Akizungumza na wananchi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya
sekondari Chato, ametoa wito kwa kila mtanzania
kuchapa kazi kwa juhudi ili nchi iondokane na
utegemezi wa misaada ya wafadhili ambayo
huambatana na masharti.
Dkt. Magufuli amesema jukumu kubwa lililo
mbele ya watanzania kwa sasa, ni kushikamana
na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja
ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi
mahali pake pa kazi.
"Kwa hiyo ni lazima tujisimamie sisi wenyewe, na
tukijisimama sisi wenyewe kwa kila mmoja
kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi
afanye kazi kwelikweli, kama ni mkulima afanye
ukulima wake kwelikweli, kama ni
mfanyabiashara afanye biashara kwelikweli,
kama ni mfugaji afuge kwelikweli, kama ni mvuvi
avue kwelikweli, Tanzania hii tutavuka" Amesema
Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli alisema serikali yake
imeamua kuchukua hatua kudhibiti nidhamu
serikalini, kwa kuhakikisha inawachukulia hatua
watumishi wa umma wanaolisababishia taifa
upotevu mkubwa wa fedha, na ameahidi kuwa
hatua hizo maarufu kwa jina la "Kutumbua
Majipu" zitaendelea kuchukuliwa hadi tatizo hilo
likomeshwe.
Dkt. Magufuli pia amekumbusha viongozi wote
wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,
Makatibu Tawala na Wakurugenzi, kutekeleza
wajibu wao ipasavyo na ameweka bayana kuwa
mahali popote ambapo hapatakuwa na ufanisi,
kiongozi husika atakuwa amedhihirisha kuwa
hatoshi kuendelea na wadhifa aliopewa.
Rais Magufuli amewapongeza walimu kote nchini
kwa kufanya kazi nzuri ya kufundisha, licha ya
changamoto ya ongezeko kubwa la wanafunzi
waliojiunga darasa la kwanza mwaka huu, lakini
ametaka Wazazi na kamati za shule kushirikiana
na walimu kuwasimamia wanafunzi ili waweze
kufanya vizuri katika masomo yao.
"Niziombe kamati za shule zote Tanzania nzima,
kama haziwezi kusimamia nidhamu ya wanafunzi
shuleni, zile kamati za shule zijiuzulu. Lakini pia
kama wewe ni Mwalimu Mkuu, shule yako kila
siku inatoa divisheni ziro nyingi kila mwaka, sioni
sababu ya wewe kuendelea kuwa Mwalimu
Mkuu" Alisisitiza Dkt. Magufuli.
Kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa, Rais Magufuli
amesema uhakiki mdogo uliofanywa hivi karibuni,
umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa
wakilipwa shilingi bilioni 1 na milioni 800, na
kwamba ni matarajio kuwa uhakiki unaofanywa
nchi nzima utaisaidia serikali kubaini wafanyakazi
hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi
za watanzania.
Ametolea mfano wa mfanyakazi mmoja wa
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ambaye
alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17, na
kueleza kuwa mfanyakazi huyo atafikishwa
mahakamani.
Pia Rais Magufuli amesema serikali yake
imejiandaa kuboresha maslai ya wafanyakazi kwa
kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi
asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo, lakini
amesema kwa wale wanaolipwa mishahara
mikubwa ambayo inafikia hadi shilingi milioni 40,
itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha
mshahara usiozidi shilingi milioni 15.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top