Uchaguzi wa zanzibar waikosesha Tanzania msaada wa trillion 1.
Sheria ya matumizi ya mitandao 'Cyber Crime
Act ya mwaka 2015' pamoja na kurudiwa kwa
uchaguzi wa Zanzibar kumefanya Marekani
kupitia kwa shirika lake la ufadhili kutangaza
kuzuia misaada yake ya kimaendeleo nchini
yenye thamani ya dola 472.8 milioni
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Shirika la
Changamoto za Milenia (MCC) imesema
Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili
kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo.
Mambo yanayolalamikiwa na shirika hilo ni
pamoja na serikali kutochukua hatua za
kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na uguru
wa kujieleza pamoja na utekelezwaji wa sheria
ya uhalifu wa mitandao.
Aidha MCC imesema huwa inazingatia na kutilia
mkazo demokrasia na kujitolea kwa nchi ili
kufanikisha uchaguzi uwe huru na wa haki.
Fedha ambazo zimekuwa zikitolewa na MCC
zimekuwa zikisaidia miradi mbalimbali ya
kimaendeleo maji, umeme na barabara hasa
maeneo ya vijijini ambapo kwa awamu ya kwanza
serikali ilipokea Dola 698.
Chanzo BBC.
0 comments :
Post a Comment