Breaking News
Loading...

Advert

Friday, March 25, 2016

Kukithiri kwa ujangili hapa nchini TANAPA sasa kuimarisha kujiimarisha kijeshi.soma zaid.

Wahifadhi na Watendaji wa Shirika la Hifadhi ya
Taifa la TANAPA,wameonywa kuwa mafunzo ya
kijeshi yanayoendelea hivi sasa kama hayataenda
sambamba na uadilifu na nidhamu,yatakuwa
hayana tija katika mapambano dhidi ya vitendo
vya ujangili vilivyoshamiri katika hifadhi zote za
taifa nchini,na kutishia kuiuwa sekta ya utalii.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Naibu
Kamishna wa Polisi Paul Chagonja,ameyasema
hayo kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake
na Mshauri wa Mgambo wa Mkoa huo Kanali
Alex Ntazi,wakati wa ufungaji wa mafunzo ya
kijeshi kwa wahifadhi na waekolojia kwenye pori
la akiba la Mlele mkoani humo,na kwamba
TANAPA izingatie kutoa mafunzo hayo kwa
watendaji wake ili kuweza kufikia malengo ya
kulinda hifadhi hizo wakiwa na jeshi usu (para
military
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa
mafunzo hayo yaliyozingatia matumizi bora ya
silaha, ukakamavu na sheria,wamesema mafunzo
yamewatia hali kubwa ya kwenda kupambana na
majangili,ambao hawana nia njema na raslimali
za Nchi hii,ambazo ni kivutio kikubwa cha watalii
na hivyo kuliingizia Taifa mapato makubwa.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top