Breaking News
Loading...

Advert

Friday, March 25, 2016

Ufisadi Spika wa Bunge job ndugai atajwa Ngorongoro soma zaid.

SPIKA wa Bunge Job Ndugai ametajwa katika
kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na
kuisababishia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
(NCAA), upotevu wa Dola za Marekani 66,890
sawa na Sh. Milioni 133.7
Washitakiwa katika kesi hiyo ni Mhifadhi Mkuu
wa zamani wa NCAA, Benard Murunya ambaye
pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki
(EALA), Meneja wa Utalii wa NCAA Veronica
Funguo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Cosmas
ya Uwakala wa Usafirishaji Salha Issa.
Kesi hiyo iliendelea jana mahakamani hapa kwa
shahidi wa kwanza wa Serikali ambaye ni Kaimu
Mhasibu Mkuu wa NCAA,Sezari Semfukwe
kuhojiwa na Wakili wa utetezi Joseph Boniface
mara baada ya kumaliza kutoa ushahidi.
Akihojiwa na Wakili Boniface, Shahidi alidai
mbele ya Hakimu ya Patricia Kisinda wa
Mahakama ya wilaya ya Arusha, kwa mujibu wa
nyaraka Murunya aliithinisha malipo ya Dola za
Marekani 66,890 kwa Kampuni ya Uwakala ya
Cosmos ambayo haikufanya kazi husika.
Alidai kuwa malipo hayo yalikuwa kwa ajili ya
Safari ya Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii
Ezekiel Maige, Murunya na Msaidizi wa Waziri
Egidius Muyungi ambao hawakutumia tiketi za
Kampuni ya Uwakala ya Cosmos.
Badala yake Aalidai malipo mengine kupitia hundi
namba 310/0379 ya Oktoba 29, Mwaka 2011 na
Tranformer Invoice namba 5609 ya Septemba 7,
Mwaka 2011 yenye Dola za Marekani 66,890
yalilipwa kwa Antelope Tours& Traveling kwa
tiketi ya Waziri Maige, Murunya, Muyungi na
kusafiri kwenda Marekani.
“Baada ya kupata taarifa kuwa huduma
haikutolewa Mhifadhi Mkuu aliandika barua ya
kutaka kujiridhisha kama huduma ilitolewa na
Kampuni ya Cosmas au haikutolewa,” alidai
shahidi huyo wa Serikali ambaye ofisi yake
inahusika na malipo na kumbukumbu zote za
fedha.
Hata hivyo Wakili wa Utetezi Boniface alimpatia
kusoma barua ya Mhifadhi Mkuu kwenda
Kampuni ya Cosmas iliyokuwa ikionyesha malipo
yalivyofanywa kwa kampuni hiyo lakini huduma
haitolewa.
Katika hatua hiyo hiyo Wakili Bonaface alimpatia
tena shahidi barua yenye majibu kutoka Kampuni
ya Cosmas kwenda kwa Mhifadhi Mkuu ambapo
shahidi aliisoma na kueleza kuwa, Kampuni ya
Cosmas ilikiri kupokea fedha lakini haikutoa
huduma.
Alidai kwa mujibu wa barua ya Kampuni ya
Cosmas waliahidi kutoa tiketi nyingine kwa ajili
ya safari Murunya, Naibu Spika Job Ndugai, Peter
Makutiani, Machumu na Kamamba.
“Hawa walisafirishwa na Kampuni ya Uwakala ya
Cosmas na hawana uhusiano na malipo ya
awali,” alidai Shahidi aliyemaliza kutoa ushahidi
wake jana akiongozwa na Wakili wa Hamidu
Sembano anayesaidiana na Wakili Mwandamizi
Rehema Mteta.
Awali mahakamani hapo Wakili wa Utetezi
Boniface aliwasilisha ombi la kujitoa kumtetea
mshitakiwa wa kwanza Murunya kutokana na kile
alichodai kuwapo kwa mawasiliano hafifu baina
yao.chanzo mtanzani.co.tz

0 comments :

Post a Comment

Back To Top