Breaking News
Loading...

Advert

Friday, March 25, 2016

Zitto na Hussein Bashe wahojiwa na Takukuru kwa tuhuma za Rusha kwenye kamati yao.soma zaid.

Muda mfupi baada ya taarifa za kashfa hiyo
kuwa wazi, Zitto na mwenzake wa Nzega Mjini,
Hussein Bashe ambao ni wajumbe wa Kamati ya
Huduma za Jamii, walimuandikia barua Spika wa
Bunge, Job Ndugai kujiondoa kwenye nafasi zao
ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
By Julius Mathias, Mwananchi jmathias@
mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Siku tatu baada ya kuibuka kwa
kashfa ya rushwa miongoni mwa wajumbe wa
Kamati za Kudumu za Bunge, Taasisi ya Kuzuia
na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemuita
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kumhoji.
Muda mfupi baada ya taarifa za kashfa hiyo
kuwa wazi, Zitto na mwenzake wa Nzega Mjini,
Hussein Bashe ambao ni wajumbe wa Kamati ya
Huduma za Jamii, walimuandikia barua Spika wa
Bunge, Job Ndugai kujiondoa kwenye nafasi zao
ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
Zitto alithibitisha kupata wito kutoka makao
makuu ya Takukuru ili kuhojiwa juu ya sakata hilo
na akapongeza kuwa endapo vyombo vya Serikali
vitakuwa makini kushughulikia tuhuma zote
zinazoelekezwa kwa wanasiasa na watumishi
wengine wa umma, itasaidia kuongeza uwajibikaji
na kupunguza uzushi kwa wananchi.
“Nimepata wito huo kupitia Ofisi ya Bunge.
Nasikia Bashe ameitwa pia. Nafurahi wito wetu
wa uchunguzi umechukuliwa kwa uzito
unaostahili na tutatoa ushirikiano wote kwa
vyombo vya uchunguzi ili kumaliza zoezi hili kwa
haraka na kwa ufanisi,” alisema Zitto.
Alipotafutwa Bashe ili kupata ukweli wa kuitwa
kwake, ingawa hakutimiza ahadi yake, alisema:
“Sipo kwenye nafasi nzuri ya kuzungumza hivi
sasa.”
Mpaka jana, wakati Takukuru ikiendelea kuwahoji
wanasiasa na watendaji wa mashirika yaliyotajwa
kuhusika kutoa rushwa ili kubadili maoni ya
wajumbe juu ya utendaji wao, wabunge wawili
walithibitika kuitwa na Takukuru.
Tuhuma hizo zimekwenda sambamba na Ndugai
kuwaondoa wenyeviti wa kamati za Ardhi,
Maliasili na Utalii; Nishati na Madini; Uwekezaji
na Mitaji ya Umma huku ile ya Hesabu za
Serikali za Mitaa (LAAC) na Huduma na
Maendeleo ya Jamii lakini akisema ni uhamisho
wa kawaida.
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino
Mlowola, bila kuingilia uchunguzi unaoendelea,
alithibitisha kuwaita wabunge hao na watendaji
wa mashirika waliohojiwa.
“Hili ni suala la uchunguzi. Bado linaendelea
hivyo si wakati muafaka kutaja watu waliohojiwa
mpaka sasa ingawa mahojiano yanaendelea. Kazi
ikikamilika utapata taarifa kamili,” alisema
Mlowola.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top