Watumish hewa 169 wagundulika mkoani kigoma ni baada ya agizo la Raisi.soma zaidi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia
Jenerali Emanuel Maganga amewataka
wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote
waliopo katika halmashauri zote kutaja
kiasi cha fedha kilichotumika kuwalipa
mishahara watumishi hewa 169 kwa
kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Akiongea na waandishi wa habari,
Brigedia Jenerali Emanuel Maganga
alisema kuwa agizo hilo ni kufuatia agizo
la Mheshimwa Rais Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli la kufanya uhakiki wa
watumishi katika halmashauri zote ili
kuwabaini watumishi hewa wanaolipwa
mishahara kinyume na utaratibu za
utumishi.
Alisema katika hao watumishi hewa 169
waliowabainika wapo ambao
walishafukuzwa kazi, wapo ambao
wameshafariki na wengine hawana sifa za
kuwa watumishi wa umma.
Mhe. Maganga alisema kuwa suala la
kuwa na wafanyakazi hewa ni wizi ambao
hauwezi kuvumilika na wizi wa kuibia
wanyonge hauwezi kuvumilika.
"Hakuna anayeweza kuvumilia wizi wa
waziwazi kiasi hiki unaofanywa na baadhi
ya watumishi wasiowaaminifu, wale wote
watakaobainika wajiandae kwani hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao"Alisema
Maganga.
Alisema kuwa fedha walizokuwa wakilipwa
watumishi hao hewa kwaajili ya mishahara
zinatakiwa kurudi zote, pia wakurugenzi
wawafute watumishi hao hewa kwenye
orodha ya malipo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa sasa
hivi katika serekali hii ya awamu ya tano
hakuna kufanya kazi kwa mazoea.
Alizitaja halmashauri zenye watumishi
hewa kuwa ni halmashauri ya kasulu
watumishi 78,halmashauri ya Kigoma
23,Manispaa ya Kigoma Ujiji
29,halmashauri ya Buhigwe 11,Uvinza
19,kibondo 5,ofisi ya Mkuu wa Mkoa 4 na
halmashauri ya Kakonko hakuna mtumishi
hewa.
0 comments :
Post a Comment