Mwenyekiti wa uchaguzi zanzibar asema maandalizi ya uchaguzi yamekamilika.
kiongea na Waandishi wa Habari Visiwani humo
Mwenyekiti wa tume hiyo Jecha Salim Jecha
amewataka Wazanzibar kutumia nafasi hiyo
kuwachagua viongozi wanaowataka kwa ajili ya
maendeleo ya wananchi wa visiwa hivyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi
Zanzibar ZEC, Salum Kassim Ali amesema zoezi
la usambazaji wa karatasi za kupigia kura katika
vituo vya kupigia kura 1583 uchaguzi wa marudio
Zanzibar ambao utafanyika kesho unaanza leo.
Salum amesema kwamba zoezi hilo linaanza leo
kuepuka uchelewashaji ambao unaweza
kujitokeza na kuainisha kuwa tume imekuwa
ikifanya kazi kwa uangalifu mkubwa ili kuepuka
ukiukwaji na nafasi ya kucheza rafu katika
uchaguzi huo.
Kulingana na Mkurugenzi wa uchaguzi kura za
kupigia kura zilichapishwa nchini Afrika Kusini
kwa gharama ya dola za kimarekani 226,000
ikiwa ni pamoja na gharama za usafirishaji wa
karatasi hizo za kupigia kura ambazo idadi yake
ni 503,850.
0 comments :
Post a Comment