Wazir mkuu awaagiza polisi kuwakamata watumishi wanne kagera.
Akitoa amri ya kukamatwa kwa Watumishi hao
Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Festo Kiswaga,
aliamuru maafisa hao wanne ambao ni Afisa wa
Mifugo wa wilaya ya Misenyi, Steven Makula,
Afisa Mifugo, Kata ya Kakuru, Eric Kagoro,
Meneja wa Ranchi Martin Ladslaus, pamoja na
Msaidizi wake kedmund Aloyce.
Akiwasomea tuhuma zinazowakabili watumishi
hao ni pamoja na kusingizia kuwa wametumwa
na uongozi wa juu kukodisha ranchi hiyo lakini
pia ikiwa ni pamoja na kuchukua fedha ambazo
walidai ni tozo la kuingiza mifugo katika ranchi
hiyo.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amependekeza
vyombo vya ulizn ina usalama wilayani humo
ikiwemo Takukuru kufanya uchunguzi wa kina juu
ya Watumishi hao na nedapo watabaika kuwa na
tuhuma za kujibu wafunguliwe mashataka mara
moja
Hivi karibuni Waziri Mkuu alifuta vitalu saba
vilivypo katika ranchi ya Misenyi, ikiwa ni pamoja
na kitalu namba moja,Kitalu namba tano, kitalu
namba saba , kitalu namba tisa, kitalu namba
kumi,kitalu namba 11, pamoja na kitalu namba 12
baada ya kubainika na kujihusisha na kuingiza
Ng'ombe kutoka nchi Jirani.
Tags: Mkuu wa Wilaya ya Misenyi
▪ Festo Kiswaga
▪ i Afisa wa Mifugo wa wilaya ya Misenyi
▪ Steven Makula
▪ Afisa Mifugo
▪ Kata ya Kakuru
▪ Eric Kagoro
▪ Meneja wa Ranchi Martin Ladslaus
▪ kedmund Aloyce.
▪
0 comments :
Post a Comment