Rais john pombe maguful awataka watanzania wote kuwa wamoja.
Rais Magufuli ametoa wito huo leo katika Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika
wa Azania Front Jijini Dar es salaam, ambako
amesali ibada ya Pasaka pamoja na waumini wa
kanisa hilo.
Amesema Mwenyezi Mungu alimtoa mwanaye
wa pekee Yesu Kristo kuja kuikomboa dunia bila
kuwabagua wanadamu, vivyo hivyo nasi
binadamu tunapaswa kutobaguana, iwe kwa dini
zetu, makabila yetu, mitazamo ya kisiasa na hata
rangi zetu.
Aidha, Rais Magufuli amewakumbusha
watanzania kufanya kazi kama ambavyo vitabu
vitakatifu vinasisitiza umuhimu wa kufanya kazi,
na amebainisha kuwa Tanzania yenye neema
inawezekana endapo kila mtu atazingatia
kufanya kazi.
“Tukifanya kazi hatuhitaji hata misaada kutoka
nje, nchi hii ina neema nyingi. Kwa kweli
tukifanya kazi kwa bidi nchi yetu inapaswa kuwa
inatoa misaada kwa nchi nyingine na sio kuomba
misaada kutoka nchi nyingine” Amesisitiza Dkt.
Magufuli.
Rais Magufuli ambaye amesali kwenye kanisa
hilo kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
lakini ikiwa ni mara yake ya nne kusali katika
kanisa hilo hata kabla ya kuwa Rais, amewaomba
watanzania kuendelea kuliombea Taifa lao na pia
kumuombea yeye ili afanikiwe kutekeleza jukumu
kubwa na zito la kuiongoza nchi.
Pamoja na kuongoza maombi ya kumuombea
Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli
waliohudhuria ibada hiyo, Askofu Mkuu wa KKKT
Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt. Alex
Malasusa amempongeza Rais Magufuli kwa tabia
yake ya kupenda kuhudhuria ibada na kuwasihi
viongozi wengine kupenda ibada.
Askofu Malasusa ameuelezea ufufuo wa Yesu
Kristo kuwa jambo la kuleta matumaini, na hivyo
amepongeza mwelekeo wa nchi kwa sasa, huku
akisema Kanisa linaona matumaini kwa Taifa.
0 comments :
Post a Comment