Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, March 27, 2016

Hivi serikali kukataa kutekeza meno ya tembo ina nia ya kukomesha ujangili nchini? soma zaid.

mko hilo limetolewa hivi karibuni na Waziri wa
Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe
akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini
Bw. Mark Childress alipotembelewa na balozi
huyo ofisini kwake kujadili maendeleo ya sekta
ya Maliasili nchini.
Prof. Maghembe alisema hayo baada Balozi huyo
wa Marekani hapa nchini kutoa pendekezo kwa
Serikali ya Tanzania kuchoma sehemu meno ya
tembo yaliyohifadhiwa ili kutoa ujumbe mzito
duniani juu ya dhamira ya Serikali kukomesha
biashara hiyo haramu.
"Naomba niweke wazi kuwa kwa sasa hatupo
tayari kuteketeza meno haya, tunaweza
kuyatumia kwenye tafiti za kisayansi au vielelezo
kwa ajili ya kesi za ujangili ambazo zipo
mahakamani na nyingine ambazo bado
zinafanyiwa uchunguzi" Alisema Prof.
Maghembe.
Zipo nchi mbalimbali duniani ambazo zimechukua
hatua ya kuteketeza meno yake ya tembo
yaliyohifadhiwa ikiwemo nchi jirani ya Kenya na
Malawi ambapo inaaminika kuwa kufanya hivyo ni
njia mojawapo ya kushawishi Ulimwengu
kukomesha biashara hii haramu ya meno ya
tembo.
Nchi nyingine ni Chad, Ubelgiji, Ufaransa, China,
India, Marekani na Ureno.
Kwa upande wa nchi ambazo zina msimamo
sawa na Tanzania katika kuendelea kuhifadhi
meno yake ya Tembo ni pamoja na Afrika ya
Kusini, Botswana na Zimbabwe.
Akizungumzia kuhusu kuendeleza sekta ya
Maliasili nchini, Prof.Maghembe amemuomba
Balozi wa Marekani Bw. Mark Childress
kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika
kukuza sekta hiyo kwa kuleta wawekezaji
mbalimbali kutoka Marekani kuja kuwekeza
Tanzania pamoja na kusaidia kwenye
mapambano dhidi ya Ujangili.
Aliongeza kuwa Tanzania ina fursa nyingi
ambazo zinahitaji uwekezaji mkubwa ikiwemo
hoteli za kitalii, fukwe za kisasa na kuendeleza
vivutio mbalimbali vilivyomo hapa nchini.
Prof. Maghembe amemshukuru balozi huyo kwa
misaada mbalimbali kutoka Serikali ya Marekani
ya kuendeleza sekta ya Maliasili nchini ukiwemo
wa hivi karibuni wa mbwa maalum (Snifer Dogs)
kwa ajili ya kusaidia utambuzi wa rasilimali za
Maliasili zinazoweza kutoroshwa nje ya nchi
kupitia bandari na viwanja vya ndege.
Katika taarifa iliyowasilishwa kwenye kikao baina
ya Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe
na Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark
Childress imeonesha kuwa katika kipindi cha
miaka mitano iliyopita Serikali ya Marekani
imetoa misaada mbalimbali ambayo jumla yake
ni dola za kimarekani Milioni 41.35 katika
kusaidia eneo la uhifadhi hapa nchini.
Akizungumzia mahusiano baina ya Tanzania na
Marekani Balozi Mark Childress alimueleza Prof.
maghembe kuwa Serikali ya Marekani
itaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya
nchi hizi mbili ambapo pia ofisi yake ya ubalozi
imeshatafuta wadau mbalimbali ambao wapo
tayari kusaidia fedha, vifaa na mafunzo kwa ajili
ya kuimarisha uhifadhi na mapambano dhidi ya
ujangili.chanzo east africa television.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top