serikali imeandaa mikakati ya kupunguza tatizo la ajira hapa nchini.soma zais.
Mkurugenzi msaidizi Taasisi ya soko la ajira
Ofisi ya Waziri mkuu kazi, Vijana, Ajira na
wenye ulemavu Ahmed Makbel
Hayo yamesemwa na mkurugenzi msaidizi wa
Taasisi ya Soko la Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Ahmed Makbel
wakati akizungumza na henura blog.spot.com kuhusu
mikakati mbalimbali na hatua zilizoanza
kuchukuliwa ili kuhakikisha inawainua vijana
kiuchumi.
Makble amezitaka taasisi zisizo za kiserikali
kushirikiana na Serikali ili waweze kutekeleza
maagizo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli na
kuhakikisha vijana wanafanya kazi zenye staha
na kipato kizuri pamoja na mazingira mazuri ya
kazi.
Mkurugenzi huyo amesema serikali imeanza
kufanyia kazi baadhi ya mapendekezo ya wadau
wa maendeleo kuhusu kuwainua vijana kuanzia
kwenye vipato vyao vya kila siku sambamba na
kuhakikisha fedha mbalimbali zinazotolewa na
serikali ziwafikie walengwa wa mifuko hiyo.
Makbel ameongeza kuwa wahusika wakuu wa
serikali kuanzia ngazi ya mtaa watoe mazingira
rafiki kwa vijana ili waone wao ni sehemu kubwa
yakuchangia pato la taifa na serikali kuu
wameanza vikao vya pamoja ili waone
wanatekeleza vipi mipango ya kukuza uchumi wa
vijana.
0 comments :
Post a Comment