Rais mteule wa zanzibar Dk.shei kesho anatarajiwa kuapiswa.soma zaid.
Rais Mteule wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein
anatarajiwa kuapishwa alhamisi asubuhi ambapo
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Othman Makungu
atamuapisha katika sherehe zitakazofanyika
uwanja wa Amani.
Kwa mujibu wa Makamu wa pili wa Rais Balozi
Seif Ali Iddi ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati
ya sherehe ya kitaifa amesema maandalizi
yanaendelea vizuri ambapo ametembelea uwanja
wa Amani na kushuhudia harakati za sherehe
hizo ambazo zitashirikisha vikosi vya ulinzi na
usalama huku Balozi akiwataka Wazanzibar
kujitokeza kwa wingi kushuhudia kuapishwa kwa
Dkt.Shein.
Balozi Seif Ali Iddi akizungumzia uchaguzi mkuu
uliomalizika juzi amesema Serikali imeridhika na
jinsi uchaguzi huo ulivyosimamiwa,kwa vile
ulikuwa wa amani na amewataka wananchi
kuacha fikra na mazungumzo yasiyo na tija na
sasa kushughulika na kazi za maendeleo kwa vile
uchaguzi umekwisha na Rais ameshapatikana
pamoja na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Dkt.Shein ambaye ni Rais Mteule wa awamu ya
saba anaapishwa kuwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi baada ya
kushinda uchaguzi wamarudio wa jumapili kwa
ushindi wa asilimia 91.4 na kuwaacha wapinzani
wake kwa kiwango kikubwa.chanzo radio one sterio
0 comments :
Post a Comment