Wilaya ya handeni imetimisa kauli ya hapa ni kazi tu baada ya kufikia lengo la elinu bure.soma zaidi.
Wilaya ya Handeni imevuka lengo la uandikishaji
wanafunzi kuanzia darasa la awali hadi la
kwanza kutoka watoto 7,000 hadi kufikia zaidi ya
21,600 na hivyo kusababisha ongezeko la mahitaji
ya Madawati na Madarasa katika shule mbali
mbali wilayani humo.
Akizungumza na ITV wilayani
Handeni,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
hiyo Luiza Oswin amesema hatua hiyo ni
utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli
aliyefuta ada na michango mbali mbali katika
Shule za Msingi na Sekondari kisha kuwahimiza
wazazi kuwaandikisha watoto wao shule ili
kuondoa visingizio vya kukosa ada na michango
mbali mbali wanayotozwa wazazi.
Kufuatia hatua hiyo Mkurugenzi huyo
amewaagiza viongozi wa Serikali za Vitongoji na
Viijiji kufanya tathmini katika kila Shule ili kupata
takwimu halisi za mahitaji ya Madawati kufuatia
Halmashauri yao kuomba kibali kwa Mkuu wa
Wilaya cha kukata Miti ili iweze kutumika
kutengeneza Madawati huku wakisubiri jibu
kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI)kuhusu suala la kuwaongezea idadi
ya Walimu katika Shule hizo.chanzo itv.
0 comments :
Post a Comment