Upelelezi dhidi ya ufisadi wa mil.83.5 mabasi yaendayo kwa kasi(DART) wakamilika.soma zaod.
Upelelezi wa kesi ya kuisababishia serikali
hasara ya Sh milioni 83.5 inayowakabili mabosi
watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka
(DART), akiwemo Mtendaji Mkuu wa mradi huo,
Asteria Mlambo, umekamilika.Wakili wa serikali,
kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (Takukuru), Stella Mafuru alidai hayo
jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi.
Hakimu Shahidi aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 12
mwaka huu itakapotajwa kwa ajili ya kuwasomea
washtakiwa maelezo ya awali. Kesi hiyo ilitajwa
mbele ya Hakimu Shahidi kwa kuwa, Hakimu
Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage anayesikiliza kesi
hiyo, hakuwepo.Mbali na Asteria, washitakiwa
wengine wanaokabiliwa na mashitaka hayo ya
uhujumu uchumi ni Mkurugenzi wa Fedha na
Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa
mradi huo, Francis Kugesha na Mkurugenzi wa
kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe.Inadaiwa
kati ya Septemba Mosi na Oktoba Mosi mwaka
2013, Kinondoni Dar es Salaam, Asteria, Katale
na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo,
walishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri na
kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 83.5 chanzo TMs fm.
0 comments :
Post a Comment