Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, March 3, 2016

Utumbuaji majipu wampa jina mpya wazir mkuu.soma zaid.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepewa jina jipya
la Kisukuma na kukabidhiwa zana nyingine
muhimu katika vita ya kupambana na ufisadi
nchini maarufu kwa jina la kutumbua majipu.
Kuanzia juzi, Waziri Mkuu Majaliwa atakuwa
akifahamika kwa jina lingine la Masanja,
alilopewa na Wazee wa Kisukuma wa Lamadi
wilayani Busega katika mkoa wa Simiyu. Kabla
ya kuwahutubia maelfu ya wakazi wa Lamadi juzi
jioni, wazee hao walimvisha Waziri Mkuu vazi la
kijadi la Kisukuma akiwa katika kigoda,
wakamkabidhi usinga, ng’ombe wawili na mkuki
ambao walimueleza kuwa kazi yake ni
kuendeleza vita ya ufisadi kwa kuutumia
kutumbua majipu.“Tunakukabidhi usinga na huu
mkuki utumike kutumbua majipu kwa sababu kazi
hii unaifanya vizuri hadi sasa, kwa hiyo uendelee
kutumbua majipu. Na kwa kuanzia sasa,
tunakupa jina la kwetu, kwa sababu wewe ni
kijana wetu, utaitwa Masanja,” alisema Mchele
Malale kwa niaba ya wazee wenzake.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top