Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, March 3, 2016

Waziri mkuu atoa siku kumi kwa watumishi wa busega.

aziri mkuu Kasim Majaliwa ametoa siku kumi
kwa watumishi wote wa halimashauri ya wilaya
ya Busega akiwemo mkurugenzi wa Halimashauri
hiyo Hamisi Yuna wanaoishi wilayani Magu
kuhakikisha wanahamia wilayani hapo ifikapo
march kumi na tano mwezi huu.
Waziri mkuu ametoa agizo hilo alipokuwa
akiwahubia wananchi wa kijiji cha Lamadi katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji
cha Kisesa.
Katika hatua nyingine waziri mkuu amewaonya
wazazi wote katika wilaya hiyo watakothubutu
kuwaachisha masomo kwa lengo la kuwaozesha
waache mara moja kwani atakayebainika katika
uongozi huu wa awamu ya tano atakiona cha
moto.
Awali mbunge wa viti maalumu mkoa wa Simiyu
Ester Midimu amemuomba waziri mkuu
kumukumbisha rais magufuri ahadi yake aliyotoa
ya kila kata kupewa shilingi milion hamsini ili
wananchi waweze kujinasua kwa kuanzisha
miradi.chanzo itv.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top