Wabunge wanaotuhumiwa kupokea Rushwa sasa kuchunguzwa na Takukuru.soma zaid.
Wabunge wamevitaka vyombo vya kuichunguzi
kuhakikisha vinazifanyia kazi tuhuma za rushwa
zinazowakabili baadhi ya wabunge kwani ni
dhahiri zinashusha hadhi ya Bunge na kuwafanya
wananchi kutokuwa na imani na wawakilishi wao.
Katika mahojiano maalum na ITV kwa nyakati
tofauti jijini Dar es Salaam wabunge hao kutoka
majimbo ya Mtera,Nyamagana,Magomeni
Visiwani Zanzibar wamesema uwepo wa tuhuma
hizo kwa wabunge waliopewa dhamana kubwa ni
fedheha kwa Bunge, huku wakitaka hatua stahiki
kuchukuliwa kama tuhuma hizo zitabainika.
Maafisa wa Bunge wanasema moja ya hatua za
awali waliokwisha kuzichukua ni pamoja na
kuwavua uwenyeviti wa kamati za kudumu za
bunge wanaotajwa katika tuhuma hizo pamoja na
kuwahamisha baadhi ya wabunge kutoka kamati
moja hadi nyingine,nakuahidi hatua nyingine zaidi
zitafuata.
Miongoni mwa hatua zilizokwisha kuchukuliwa na
Spika wa Bunge chini ya kanuni ya 116(3) cha
kanuni za kudumu za Bunge,ni pamoja na
kufanya mabadiliko katika kamati 5 za Bunge
pamoja na kufanya mabadiliko ya wajumbe katika
kamati hizo.
0 comments :
Post a Comment