Licha ya Rais magufuli kuagiza mashine ya EFD's kutolewa bura kwa wafanya biashara hapa nchini mkuu wa kitengo cha machine ya lielekitroniki amemuweka ngumu.soma zaid.
Wakati wafanyabiashara wakisubiri kupewa bure
mashine za kieletroniki (EFD’s) kama Rais John
Magufuli, alivyosema, Mamlaka ya Mapato (TRA)
imesema kauli ya Rais ilikuwa ni mtazamo wake
na siyo agizo kama linavyopotoshwa na baadhi
ya wafanyabiashara.Mkuu wa Kitengo cha
Usimamizi wa Mashine za Kieletroniki na Kodi
Mkoa wa Kodi Temeke, Kennedy Sawaya,
aliyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa
Mwaka wa Chemba ya Wafanyabiashara,
Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA).
Alisema mashine za bure zitatolewa kwa baadhi
ya sekta na hazitawahusu wafanyabiashara
wasajiliwa wa Vat na wale wanaotegemea
kusajiliwa humo.Sawaya alitoa maelezo hayo
baada ya mmoja wa washiriki wa mkutano huo
kutaka kujua kwa nini TRA inachelewa kutoa
mashine hizo ambazo Rais Magufuli aliagiza
zigawiwe bure kwa wafanyabiashara nchini.
Akijibu swali hilo alisema: “Ulikuwa ni mtizamo
wa Rais kama TRA inaweza kufanya hivyo,
hakuna bajeti iliyoelekezwa kuzinunua mashine
hizi hata zikitolewa bure ni kwa baadhi ya sekta,”
alisema.
0 comments :
Post a Comment